BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini NBAA, imepitisha na kutangaza matokeo ya watahiniwa 5827 waliofanya mtihani kati ya terehe 04 hadi terehe 07, Agosti ile iliyotakiwa kufanyika Mwezi Mei 2020 katika ngazi mbalimbali za masomo. Mtihani hii ilihairishwa kutokana na janga la Ugonjwa wa Homa kali ya mapafu(Corona) ulioenea ulimwenguni kote.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno imebainisha kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 13 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya Pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa Hesabu (ATEC I , ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya Awali/Msingi (Foundation Level) yenye masomo matano, Hatua ya Kati (intermiediate Level), yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne.
"Watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 6,934 kati ya hao watahiniwa 1,107 sawa na asilimia 16.0 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 5,827 sawa na asilimia
84.0. Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 151 ambao ni asilimia 2.6 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 137 sawa na asilimia 2.4 wamefaulu kwa kufaulu masomo walioyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, wengine 924 sawa na asilimia 15.9 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza," alisema Maneno.
Pia alisema watahiniwa 1,214 sawa na asilimia 20.8 wamefaulu mitihani yao na kwamba watahiniwa wengine 2,492 sawa na asilimia 42.8 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali na watahiniwa 2,123 waliobakia sawa na asilimia 36.4 hawakufaulu mitibani yao.
Awali, taarifa hiyo ilieleza kuwa watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 84 kati ya hao watahiniwa 10 sawa na asilimia 11.9 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo kufanya ndani ya watahiniwa waliofanya mitihani kuwa 74 sawa na asilimia 88.1.
Pia imeelezwa kuwa kati ya watahiniwa 74 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 10 ambao ni asilimia 13.5 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku wengine 08 sawa na asilimia 10.8 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza, wengine 18 sawa na asilimia 24.3 wamefaulu huku watahiniwa 28 sawa na asilimia 37.8 wamefaulu baadhi ya masomo katika kazi hii na watahiniwa 28 waliobaki sawa na asilimia 37.8 hawakufaulu mitihani yao..
Aidha, katika hatua ya Kati, waliojisaliwa walikuwa 3,721 kati ya hao watahiniwa 618 sawa na asilimia 16.6 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 3,103 sawa na asilimia 83.4 Kati ya watahiniwa 3,103 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 31 ambao ni asilimia 1.0 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 99 sawa na asilimia 3.2 wamefaulu kwa kufaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma.
Alisisitiza wengine 528 sawa na asilimia 17.0 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza. Kwa ujumla watahiniwa 658 sawa na asilimia 21.2 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 1,457 sawa na asilimia 47.0 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 988 waliobakia sawa na asilimia 31.8 hawakufaulu mitihani yao.
Katika hatua ya mwisho, watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 2,245 kati ya hao watahiniwa 340 sawa na asilimia 15.1 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo hiyvo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 1,905 sawa asilimia 84.9.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ametoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment