Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna akizungumza. Kuhusiana namna wqlivyojipanga katika mpango wa Dunduliza kwa wananchi kuchangia kidogo kidogo ili kuweza kujiunga na huduma za matibabu ya NHIF.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga akishikana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna Mara baada kusaini makubaliano katika uzinduzi wa mpango wa Dunduliza uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga (katikati) wakionesha mabakubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja kati ya NHIF na Benki ya NMB Mara baada ya kusaini makubaliano.
*Wananchi kujiunga na huduma za matibabu za NHIF
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Benki ya NMB wamezindua mpango unaojulikana Dunduliza unaowezesha wananchi kudunduliza fedha kidogo kidogo za mchango wa bima ya afya na hatimaye kufanikisha kuchangia kiwango kinachotakiwa na kujiunga na huduma za bima ya afya kupitia NHIF.
Uzinduzi huo umefanyika Dar es Salaam ambapo pia uzinduzi umeambatana na kusaini makubaliano (MOU) kati ya NHIF na Benki ya NMB ya namna ya wateja watakavyoweza kuchangia ama kujiwekea fedha kwa ajili ya kukamilisha mchango wa huduma anazohitaji.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga amesema mpango wa Dunduliza unawezesha wananchi wa wanaojiunga na NHIF kupitia mpango wa vifurishi kuweka fedha kidogo kidogo kupitia Benki ya NMB kwa muda atachagua na atakakamilisha kiwango husika atapatiwa kadi ya matibabu na kuanza kunufaika na huduma za matibabu kupitia NHIF.
Amesema mwananchi anayehitaji kujiunga na huduma za NHIF ambaye anahitaji kuweka fedha kidogo kidogo kupitia banki ya NMB kwa muda atakaochagua na atakakamilisha kiwango husika atapatiwa kadi ya matibabu na kuanza kunufaika na huduma za matibabu kupitia NHIF.
Amesema mwananchi anahitaji kujiunga na huduma za mfuko wa Taifa wa Bima ya afya ambaye atahitaji kuweka fedha kidogo kidogo kwa muda atakaochagua ni yule anajiunga kupitia mpango wa vifurishi ambavyiuvinajulikana kwa majina ya Najali Afya, Wekeza afya na Timiza afya ambavyo pia vina mpa fursa mwananchi anayehitaji kuchangia kuchagua huduma kulingana na mahitaji yake, umri na wanufaika wanaohitaji kuwajumuisha.
Amesema mpango huu unawezesha mwananchi kujiwekea fedha kwa ajili yake Mwenyewe ama kwa ajili yake na mwenza wake na mtoto ama Watoto alionao.
Amesema mfumo huo haubagui mwananchi yoyote kulingana na aina ya simu aliyonayo na endapo atakwama katika hatua za kujisajili.
Amesema wakati mfuko unazindua mpango wa vifurushiu Novemva mwaka jana, changamoto iliyionekana ni pamoja na uwezo wa wananchi kulipa fedha zote kwa awamu moja hatua iliyoifuata Menejimenti ya mfukonkufungua milango na kuanza kushirikiana na wadau wa Taasisi za kifedha kama NMB ambayo ina wigo mpana kwa nchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ruth Zaipuna amesema anafarijika kuzinduliwa kwa mpango huo ambao anaamini utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kuwa ndani ya mpango wa NHIF lakini pia kuwajengea wananchi tabia ya kujiwekea akiba kwa matumizi yanye manufaa ya baadaye kwao.
"Afya ni kila kitu na hata kwa upande wetu sisi Benki, tunahitaji Sana wateja ambao Wana uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote na sio wa kuchujua akiba zao Benki kwenda kujitibia, niombe Sana wananchi tuutumie huu mpango kuhakikisha wengi wetu tunajiwekea fedha na hatimaye kupata kadi ya matibabu."Amesema Bi Zaipuna
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment