Wahariri wapongeza jitihada zinazofanywa sekta ya mifugo kwa kutengeneza chanjo ya mifugo.
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV
Chanjo za Mifugo kutengenezwa nchini ni hatua ya kufanya nchi kuwa na usalama wa afya ya wananchi wake.
Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi-Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel wakati alipozungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari waliokwenda katika Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Kibaha mkoani Pwani iliyopo chini ya Wakala ya Mabaara ya Veterinari Tanzania (TVLA).
Profesa Ole Gabriel amesema kuwa Sekta ya Mifugo imepiga hatua kwa kuwa na Chanjo za wanyama zinazozalishwa nchini kwa kujenga maabara za kisasa.
Amesema kuwa nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo kuwa na chanjo za wanyama ni usalama wa nchi kuliko kutegemea chanjo kutoka nje ya nchi.
"Suala la uchumi ni vita kwani kuwa na chanjo zetu kunafanya wananchi wetu kuwa salama zaidi katika kutumia mazao ya mifugo"amesema Profesa Ole Gabriel.
Aidha amesema kuwa Taasisi ya Chaanjo imepiga hatua kwa kuzalisha chanjo sita huku malengo ni kuzalisha chanjo 13 za kimkakati.
Amesema wanyama wakipata chanjo kunafanya mazao yake kuwa salama kwa afya katika Maziwa Nyama pamoja na Ngozi na hivyo kuongeza Pato la Taifa.
Taasisi hiyo imezalisha chanjo ya Mdondo, Kimeta ,Chambavu, Brucellosis,CBPP pamoja Tecoblax.
Profesa Ole Gabriel amesema wafugaji wasiwe wao wenyewe ndio wataalam wa kutibu wanyama wao wakati Watu wenye utaalam huo wapo.
"Tatizo la baadhi ya wafugaji wanakuwa wataalam hili ni tatizo na waache kufanya hivyo ili Watu wenye utaalam waweze kufanya kazi zao"amesema Profesa Ole Gabriel.
Profesa Ole Gabriel amewata TVLA na TVI kuzalisha chanjo nyingi na kuweza hata kuuza katika nchi ambazo hazitengenezi chanjo.
Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt.Furaha Mramba amesema kuwa serikali imejenga miundombinu mbalimbali katika uimarishaji wa Maabara kwa kuhakikisha chanjo za mifugo zinazalishwa hapa hapa nchini.
Dkt.Mramba amesema kuwa magonjwa ya mifugo yanaongoza kumaliza mfugo hayana dawa njia pekee ambayo imefanya serikali kujenga maabara ya Chanjo pamoja na kuweka Rasilimali Watu wenye utaalam wa kufanya hivyo.
Hata hivyo amesema kuwa mikakati iliyopo ni pamoja na kuongeza cliniki za mifugo ili kusogeza huduma kwa wafugaji.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Habari Leo Mgaya Kingoba kwa niaba ya Wahariri amesema Wahariri watakuwa wa kwanza katika kuweza kuelimisha wananchi kuhusiana na sekta ya mifugo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment