RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuifungua Skuli ya Seondari ya
John Pombe Magufuli iliopewa jina baada ya kufunguliwa leo 9/10/2020.na
(kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki
Pembe na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Dkt. Idriss Muslim Hija na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi, hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya
Skuli hiyo Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar.(Pichana Ikulu)WANAFUNZI wa Skuli ya Mpya ya Sekondari ya John Pombe
Magufuli wakishangilia wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Skuli yao
mpya ilioko katika eneo la Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar, hafla hiyo
imefanyika leo 9/10/2020.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mwanafunzi wa Kidatu cha Tano wa
Skuli ya Sekondari ya John Pombe Magufuli . Fatma Ally Othman , akitowa
maelezo jinsi ya kupima mawimbi ya maji, alipotembelea maabara ya
Fizikia, baada ya ufunguzi wa Skuli hiyo leo 9/10/2020 na kulia Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi, hafla hiyo
imefanyika leo.(Picha na Ikulu )
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.
Ali Mohamed Shein akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli Mpya
ya Sekondari ya Dkt.John Pombe Magufuli Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar,
baada ya kuifungua na kupewa jina hilo leo 9/10/2020.(Picha na Ikulu)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment