RC KUNENGE AZINDUA SAFARI YA KWANZA YA TRENI KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA ARUSHA | Tarimo Blog






Matukio mbalimbali katika picha yakimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC,) Mhandisi. Masanja Kadogosa wakati wa uzinduzi wa safari ya treni kutoka Dar es Salam kwenda Arusha, leo jijini Dar es Salaam.

Na wandishi wetu, Dar es Salaam.

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge leo Oktoba 02 amezindua safari ya kwanza ya treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Mkoani Arusha iliyokuwa imekosekana kwa takribani miaka 30 na kusababisha adha ya usafiri kwa wananchi.

Akizindua safari hiyo RC Kunenge amelielekeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri na amewapongeza TRC kwa mapinduzi makubwa na mazuri wanayoyafanya katika usafiri wa  reli.

Aidha RC Kunenge amesema, treni hiyo itasaidia wafanyabiashara na  wananchi hususani wa kipato cha kawaida kupata usafiri wa haraka na kwa bei nafuu hivyo ametoa wito Kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

Pamoja na hayo RC Kunenge ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa  Rais Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alizotoa na maamuzi yake ya kufufua usafiri wa treni.

Kwa upande wake Mkurugwnzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi. Masanja Kadogosa amesema Shirika hilo limejizatiti vyema katika kuhakikisha linatoa huduma bora na salama kwa wananchi wote


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2