Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dk. Julius Mwaiselage akizungumza na mashujaa wa Saratani ya Matiti katika mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga za Saratani wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Crispin Kahesa akizungumza jambo katika semina ya siku moja kwa mashujaa wa saratani ya matiti iliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mashujaa (wanawake waliotibiwa na kupona saratani ya matiti) na wale wanaoendelea na matibabu dhidi ya ugonjw huo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage hayupo pichani
Mashujaa (wanawake waliotibiwa na kupona saratani ya matiti) na wale wanaoendelea na matibabu dhidi ya saratani hiyo, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dk. Julius Mwaiselage na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa ORCI, Dk. Crispin Kahesa wakiinua mkono juu kama ishara ya kuishinda saratani hiyo kwa matibabu.
*Watu wa Tiba Asili na Wagaga wa Jadi wawachangamoto.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAGONJWA ya Saratani yanatibika kwa kutumia dawa kuwakatizia matibabu hayo na kuwapeleka kwenye maombi ya tiba za asili na waganga wa jadi kwani wanaweza kuwasababishia madhara makubwa zaidi ikiwemo kifo.
Jamii inaaswa kukubali wataalam wanaowatibu bila kufuata mambo ambayo hayahusiani na wataalam katika maeneo husika huku elimu inayotolewa na Taasisi hiyo imekuwa na mafanikio na kuwapata mashujaa wa Saratani ya matiti waliopona kutokana kufuata tiba sahihi na si vinginevyo.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani (Ocean Road)Dkt Julius Mwaiselage katika mafunzo kwa mashujaa wa saratani ya matiti yaliyofanyika katika Taasisi hiyo, Dkt Mwaiselage amesema mafunzo hayo yanalenga kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya saratani na jinsi ya kujikinga ambapo mwezi oktoba umetengwa mahususi katika kutoa elimu ya saratani kwa jamii katika meoneo mbalimbali.
Dkt. Mwaiselage amewataka waganga wa tiba za asili na watu wa maombezi kutowazuia wagonjwa wa saratani kuendelea kuhudhuria matibabu yao hospitali na pale wanapowapa dawa kushauriana kwanza na Daktari ili ijulikane dawa wanazotoa zinatibu ugonjwa gani.
"Wito wangu hawa wanaotoa tiba mbadala iwe ni maombi au wanaotangaza kuwa wana dawa za kutibu saratani kuacha kabisa kuwazuia wagonjwa wa saratani kuendelea na matibabu ambayo wanapatiwa na Taasisi ya Ocean Road kwani wanatupa wakati mgumu wa kuwatibu wagonjwa kutokana na kurudi hospitali wakiwa katika hatua ya tatu na nne ambayo ni changamoto kwa mgonjwa kupona"Amesema Dkt Mwaiselage.
Aidha amesema kwa sasa serikali imeboresha huduma za Afya katika Taasisi hiyo ikiwemo upatikanaji wa dawa, na vifaa tiba ikiwemo mashine za kisasa ambapo wagonjwa wanaweza kupata matibabu na kupona kabisa
Ameongeza kuwa kwa sasa huduma ya kutibu saratani ya matiti ambayo inashika nafasi ya pili kwa asilimia 15 kati ya wagonjwa wa saratani elfu 42 kila mwaka inatibika kwa kukuondoa tu uvimbe bila kukata titi lote na kwa waliokatwa titi tayari kuna Madaktari walioenda kupatiwa mafunzo nchini China na wakirudi watawafanyia upasuaji wa kurudisha titi.
Aidha katika mafunzo hayo pia kutatolewa elimu ya jinsi ya kuishi na saratani ndani ya jamii ikiwemo kunyanyapaliwa haswa kwa wale wanaokatwa titi, imani potofu kuwa saratani haiponi na matangazo ya kwenye mitandao ya uwepo wa dawa za kutibu ugonjwa wa saratani kutokana na wagonjwa wa saratani kuchukua mda mrefu kupona kwa kuzingatia taratibu za hospitali.
Hata hivyo amesema huduma za matibabu ya saratani zimeboreshwa katika kipindi hiki cha awamu ya 5 ambapo kila mwaka bajeti ya zaidi ya shilingi Bilioni 7 hutengwa kwa ajili ya dawa za saratani na kusababisha wagonjwa wa saratani kuishi kwa muda mrefu.
Dkt Mwaiselage amesema katika kipindi hiki cha mwezi mmoja cha kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa wa saratani watatoa huduma ya uchunguzi wa saratani na elimu kwa wananchi ili wajichunguze wenyewe pamoja na kuwasisitiza kuwahi hospitali mapema pindi wanapoona dalili za ugonjwa wa saratani.
Sambamba na hayo amesema baada ya kuboresha kwa huduma za Afya katika Taasisi hiyo kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 wamekuwa wakipokea wagonjwa elfu 55 kila mwaka tofauti na awali walipokuwa wanapokea wagonjwa elfu 33 huku wanaotibiwa na kupona ni asilimia 60 tofauti na awali walikuwa wanapona asilimia 20 tu.
Kwa upande wake Meneja Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani Dkt Maguha Stephon amesema sababu zinazochangia kuongezeka kwa saratani ya matiti ni pamoja na wanawake kutonyonyesha kwa muda mrefu, kuacha kunyonyesha kabla ya miaka 2, aina ya ulaji wa vyakula ikiwemo vile vya mafuta, kupata hedhi mapema na kurithi.
Dkt Maguha amesema ugonjwa wa saratani bado ni tishio Duniani ambapo kila mwaka hupatikana wagonjwa milioni 18 hivyo jamii inapaswa kujilinda dhidi ya ugonjwa wa saratani hususani ya matiti ambayo kwa kiasi kikubwa huadhiri wanawake kwa asilimia 99 na wanaume kwa asilimia 1 kwa kula vyakula vya mboga mboga, samaki kunyonyesha kwa wakati na kufanya uchunguzi wa saratani mara kwa mara.
Nao baadhi ya mashujaa wa saratani waliohudhuria katika mafunzo hayo akiwemo Halima Mwaipopo ambaye ametibiwa miaka 18 sasa kwa kukatwa titi lake amesema kwa sasa anajisikia kupona kabisa na hiyo inatokana na kuzingatia taratibu zote alizokuwa anaelekezwa na Daktari pamoja na kutokata tamaa licha ya unyanyapaa aliokuwa anaupata ndani ya jamii alijipa moyo na kumuomba Mungu.
Shujaa wa Saratani Nyakolema Silla amtoa wito kwa wagonjwa wa saratani kutokata tamaa na kuzingatia hatua zote za matibabu wanazoelekezwa na Daktari pamoja na kukubaliana na hali zao kwani itawasaidia kuishi na jamii bila kujali changamoto za kunyanyapaliwa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment