TUME YA UCHAGUZI YAFIKA KAGERA NA KUAGIZA HAYA | Tarimo Blog


Na Abdullatif Yunus MichuziTv.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefika Mkoani na Kufanya Semina na Wadau wa Uchaguzi Lengo ikiwa ni kuendelea kutoa Elimu kwa Mpiga Kura tunapoelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 28 Mwaka huu.


Akisoma Hotuba ya Utangulizi wakati wa Ufunguzi wa Semina hiyo Ndg.   Adam Mkina, ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa sera na mipango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume, Amesema kuwa Tume wakati inaendelea mipango mingine ya kuratibu na kusimamia Uchaguzi kwa kutumia Sheria za Uchaguzi, Sheria nyingine za Nchi hazijakoma hivyo Wananchi, wagombea na Vyama vya Siasa kuchukua Tahadhali kwa kujiepusha na Yale yote yanayoweza kuashiria Uvunjifu wa Amani. 


Aidha Mkina ameongeza kuwa Tume imejipanga 

Kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, unafanyika katika Misingi ya Haki, Usawa, Uadilifu kwa kufuata miongozo na taratibu zilizowekwa kisheria kwa Mujibu wa Katiba, na kwamba kila Mdau akifikisha ujumbe huu kwa Wadau wake Uchaguzi utafanyika na kumalizika kwa Amani.


Naye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semitocless Kaijage amesisitiza Juu ya Wale wote wanaofikilia kufanya vurugu zinazoweza kuharibu Uchaguzi, kuwa hawatapa nafasi, hivyo ni vyema kujipanga zaidi kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi kuanzia michakato yake ikiwa Ni sambamba na kuendelea kutoa Elimu sahihi ya Mpiga Kura, ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga Kura.


Katika Semina hiyo iliyohudhuliwa na wawakilishi wa Makundi mbalimbali yakiwemo Watu wenye Ulemavu, Wanawake, Vijana, Wazee, Viongozi wa Dini,   Asasi za Kiraia na Waandishi wa Habari, washiriki wamepata nafasi ya Kujadili mada mbalimbali zilizowasilishwa na kuuliza maswali, ambapo kupitia Makundi haya watakuwa mabalozi kwa wanaowawakilisha na kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semitocless Kaijage akisisitiza Jambo kwa Washiriki wa Semina ya Elimu ya Mpiga Kura iliyofanyika Ukumbi wa Bukoba Sekondari Mkoani Kagera

 Mtaalam wa lugha ya alama akiendelea kutoa ufafanuzi wa Mambo mbalimbali kwa kundi la watu wenye Ulemavu ambao wamehudhulia Semina hiyo katika Ukumbi wa Bukoba Sekondari wakati Tume ya Uchaguzi ilipowasili Mkoani  Kagera.

 Sehemu ya wawakilishi wa Makundi mbalimbali wakiendelea kufuatilia mada wakati wa Semina ya Elimu kwa Mpiga Kura iliyofanyika Ukumbi wa Bukoba Sekondari Mkoani Kagera.

 Ndg. Adam Mkina, Mkurugenzi msaidizi wa sera na mipango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa katika Semina ya Elimu kwa Mpiga Kura iliyofanyika Ukumbi wa Bukoba Sekondari Mkoani Kagera.

Picha ya Pamoja na mwakilishi wa kundi la Vijana.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2