Wiki ya Huduma kwa Wateja 2020: Benki ya Exim Yaahidi Ufanisi Zaidi Huduma za Kidigitali | Tarimo Blog

 

 Benki ya Exim Tanzania imeungana na ulimwengu wote kwa kutoa heshima kwa wateja na wafanyikazi wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  Wiki ya Kimataifa ya Huduma kwa Wateja inayofanyika kila mwaka mwezi Oktoba. Benki hiyo  imeahidi kuboresha zaidi huduma zake hususani zile za kidigitali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bwana Jaffari Matundu akiwa ameambatana na maofisa waandamizi wa benki hiyo walitembelea matawi kadhaa pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam ili kuzungumza na wafanyakazi pamoja na kupata mrejesho kutoka kwa wateja wa kuhusu huduma zinazotolewa na wateja wa benki hiyo.

"Kama taasisi inayotoa huduma muhimu kwa wateja, wiki hii ni muhimu kwetu Benki ya Exim kwa kuwa inatupa fursa ya kushirikiana kikamilifu na wateja wetu. Uhusiano mzuri na madhubuti na wateja wetu unabaki kuwa muhimu sana kimkakati na hatua hii inaonyesha nia yetu ya kutambua jambo hili, ”alisema Bw Matundu wakati alipotembelea tawi la Makao Makuu ya benki  hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumzia umuhimu wa utoaji wa huduma kwa ubora, Bw Matundu aliwapongeza wafanyakazi wa benki hiyo huku akionyesha kutambua namna wanavyojituma kuwahudumia wateja kwa weledi na kwa uaminifu mkubwa.

"Kila wakati tumekuwa tukitafuta njia mpya za kuwahudumia wateja wa benki ya Exim kwa weledi zaidi huku pia tukihamasisha ukuaji wa pamoja  kati yetu na wateja wetu." Alisema.

Kwa upande wake  Meneja Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo Bwana Frank Matoro alifafanua namna benki hiyo inavyojitoa katika kuwahakikishia utoaji wa huduma bora wateja wake ili kukidhi mahitaji na matarajio yao wakati wote.

"Ni muhimu kuonyesha na kuthamini thamani ya utoaji bora wa huduma kulingana na uzoefu na mahitaji ya wateja wetu, kwa kuwa vitu hivi ni viungo muhimu katika kujenga taasisi ya kifedha yenye  nguvu zaidi nchini." Alisema

Katika ziara yake kwa baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam huku akiwa ameambatana na baadhi ya maafisa waandamizi wa benki hiyo  Bw Matoro alitumia fursa hiyo kutumia na kuelezea baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo hususani zile za kidigitali yakiwemo matumizi ya kadi za benki katika kufanya miamala.

“Ili kufanya huduma zetu ziwe nzuri zaidi na rahisi kwa wateja, Exim benki tunazo chaguzi kadhaa ikiwemo kutumia huduma ya mobile bank inayohusisha matumizi ya simu za mkononi au kwa njia ya USSD, kutumia kadi zetu za benki, mtandao wetu wa POS na pia kutumia huduma za mtandaoni kupitia wavuti au programu (App) ambazo zinawawezesha wateja wetu kupata huduma muhimu za kifedha muda wote ,’’ alitaja Bw Matoro.

Kufuatia ziara hizo baadhi ya wateja wa benki hiyo ikiwa ni pamoja na kampuni za MMI Tanzania, inayojishughulisha na biashara ya mvinyo pamoja na kampuni ya  Shrijee Traders walionesha kuridhishwa kwao na huduma zinazotolewa na benki hiyo pamoja na heshima ya kutembelewa na maofisa wa benki hiyo.

"Kimsingi nimekuwa nikiridhishwa na huduma ninazopatiwa kupitia benki ya Exim ikiwemo malipo ya hundi, malipo kwa njia ya mtandao pamoja na matumzi ya kadi za malipo ambayo kiukweli zinatolewa kwa ufanisi mkubwa. Niwaombe tu benki ya Exim waendelee kuhamasisha malipo kwa njia ya kidigitali maana ni bora zaid.Ninajivunia kuhudumiwa na Benki ya Exim,’’ alisema Bw Sabalsinh Champs, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Shrijee Traders inayomiliki Supermarket ya Shrijee’s iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania, Jafari Matundu (Kulia) akiongea na mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw Bakari Mikidadi  (aliekaa) wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea tawi la benki hiyo la Exim Tower jijini Dar es Salaam  ili kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa kwa wateja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine ni pamoja na Meneja wa benki hiyo tawi la Exim Tower Bw  Vishal Ratansinh (Katikati) na Meneja Msaidizi Huduma kwa wateja wa benki hiyo Bi Rukio Chambuso.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania, Jafari Matundu (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa benki hiyo ikiwemo Idara ya Huduma kwa wateja  wakati wa hafla fupi ya kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja.

Baadhi ya maofisa wa benki ya Exim wakiongozwa na Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja Benki hiyo, Bw Frank Matoro (wa tatu kulia) wakibidhi keki kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bi Rahel Athumani ambae ni  Meneja Mauzo Msaidizi kutoka kampuni ya kuuza vinywaji ya MMI (wa nne kushoto) wakati maofisa hao walimpomtembelea mteja huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.

Maliza Kirahisi Kidigitali! Baadhi ya maofisa waandamizi wa benki ya Exim kutoka Idara ya Huduma kwa wateja akiwemo Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja Benki hiyo, Bw Frank Matoro (kushoto)  na Bw Abdalla Rashidi (Katikati) wakimuhudumia mmoja wa wateja aliefika kununua vinywaji kwenye  duka la kampuni ya vinywaji ya MMI ambayo ni mteja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Mauzo Msaidizi wa kampuni ya kuuza vinywaji ya MMI ya jijini Dar es Salaam  Bi Rahel Athumani  akifurahia keki aliyokabidhiwa na maofisa wa benki ya Exim  wakati maofisa hao walimpomtembelea mteja huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya maofisa wa benki ya Exim wakibidhi keki kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw Sabalsinh Champsi (Kushoto) ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa duka la  Shrijee’s Super market la jijini Dar es Salaam wakati maofisa hao walimpomtembelea mteja huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja

Baadhi ya maofisa wa benki ya Exim wakibidhi keki kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw Sabalsinh Champsi (Kushoto) ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa  duka la  Shrijee’s Super market la jijini Dar es Salaam wakati maofisa hao walimpomtembelea mteja huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Maofisa wa benki ya Exim wakiwa kwenye picha ya pamoja mteja wa benki hiyo Bw Sabalsinh Champsi (Katikati) ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa  duka la  Shrijee’s Super market la jijini Dar es Salaam wakati maofisa hao walimpomtembelea mteja huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Baadhi ya maofisa wa benki ya Exim wakibidhi keki kwa wawakilishi wa  kampuni ya kuuza vinywaji ya MMI ya jijini Dar es Salaam  ambayo ni mteja wa benki hiyo akiwemo Meneja Mauzo Msaidizi wa kampuni  hiyo Bi Rahel Athumani  (wa pili kulia) wakati maofisa hao walimpomtembelea mteja huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2