Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk.Edmund Mndolwa, akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro jana kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, mkoa humo, Daudi Mrindoko.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk.Edmund Mndolwa, akisalimiana na wanajumuhiya hiyo wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuwasili katika ziara ya kikazi.
Salamu zikiendelea.
Mapokezi yakifanyika.
Salamu zikiendelea.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk.Edmund Mndolwa, jana aliendelea na ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro kwa na kuzungumza na wajumbe wa Baraza la Wazazi la mkoa huo.
Mndolwa aliwapongeza wanachama na viongozi wa jumuiya hiyo kwa ushiriki wao kikamilifu katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu zilizoleta matokeo chanya kwa mkoa huo na kuibuka na ushindi wa kishindo kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Madiwani.
Pia aliwasihi watendaji wa jumuiya hiyo kuendelea kufanya kazi na kuisemea jumuiya kwa ushirikiano mkubwa na CCM.
"Nawapongeza watendaji wa Jumuiya ya Wazazi kwa kazi kubwa mnayoifanya katika kuitetea na kuipaisha jumuiya yetu, ninafahamu changamoto ni nyingi ila endeleeni kupambana;
"Pia nitoe wito kwenu wakuu wa Shule za Sekondari za Jumuiya ya Wazazi kote nchini kuhakikisha walau kila mkoa mchague katika hizo shule mojawapo iwe inafundisha masomo ya sayansi tu, lengo kuisaidia serikali na jamii yetu kupata madaktari na wataalamu wa masuala ya sayansi hata kuongeza walimu wa masomo ya sayansi" alisema Dk.Mndolwa.
Akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kilimanjaro, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Daudi Mrindoko, alimshukuru Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Dk.Mndolwa, kwa ziara hiyo inayotoa Dira ya wapi jumuiya hiyo inatakiwa ielekee katika kusaidia jamii kote nchini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment