DONALD TRUMP AJITANGAZA KUSHINDA URAIS MWAKA HUU | Tarimo Blog

Na Lusajo Frank DSJ 
RAIS wa Marekani, Donald Trump amedai kushinda uchaguzi wa Marekani licha ya kwamba matokeo ya mwisho bado hayajatangazwa licha ya hilo amesema atakwenda Mahakama ya Juu kupinga kuendelea kuhesabiwa kwa kura. 

Trump amejitangazia ushindi huo katika hotuba isiyo ya kawaida akiwa Ikulu ya White House, na kuongeza kuwa kuendelea kuhesabiwa kwa kura ni njama ya kufanya udanganyifu.

Matokeo ya awali yanaonesha Trump akiwa katika mchuano mkali na  mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden,

Mgombea wa chama cha Repulican,Trump amesema ataenda mahakamani na anataka upigaji kura wote kusimama  akionekana kumaanisha kusitisha kuhesabiwa kwa kura za posta.

Suala hilo linaweza kugeuka nyeti katika majimbo ambayo yanaendelea kuhesabu kura katika kinyang'anyiro hicho kikali. 

Timu ya kampeni ya Joe Biden imekosoa matamshi hayo ya Trump na kuyataja kuwa kashfa, na baadhi ya wanachama wa chama chake cha Repulican pia wameikosoa hatua hiyo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2