MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba Mohamed Dewji ameeleza mambo kadhaa kuelekea michuano ya kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika huku akitaja matumaini waliyokuwa nayo kuelekea michuano hiyo pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara hasa kutetea ubingwa wao.
Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mo Dewji amesema kwanza wanatoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano,kwa kuanza na Rais Dk.John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
"Kwa niaba yangu na kwa niaba ya bodi ya Simba tunawapongeza, na tunapompngeza sana Rais Magufuli.Pia tunapowangeza wabunge na madiwani na wote waliochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.Pilia pili katika mkutano wa bodi tumejadiliana na kubwa zaidi bado tuna dira wana shabaha na hatutaki kutoka kwenye reli.
"Maana yake bado tunataka kutetea ubingwa wetu, tunajua kwamba ligi ni ngumu lakini tuna zaidi ya mechi 30 zimebaki, kwa hiyo tuseme ligi bado mbichi na tumepita kwenye misuko suko , kumekuwa na hujuma hujuma lakini tumekuja kujua wapi tunahujimiwa, tunasema tumechukua hatua za haraka ili hujuma zisiendelee.
"Kwa hiyo naomba niwaambie wana Simba na watanzania shabaha yetu ni kutetea ubingwa wetu na tutapambana mpaka mwisho, na Mungu akitujaalia na kututangulia tutafanikiwa katika hilo lengo,"amesema Mo.
Aidha amesema wanafahamu kwamba droo ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika imeshatoka na wataanza kucheza na timu ya Plateua nchini Nigeria ."Tumeona droo ya klabu bingwa imetoka bado kuna kumbukumbu mbaya ya mwaka jana, kwa hiyo mwaka huu tumejipanga vizuri zaidi.
"Sasa unajua kuna advantarge na dis advantarge, kwa hii timu ambayo tunacheza nayo, advantarge kubwa ni kwenda kuanza Nigeria. Tunafahamu wale watu ni watalaam sana katika mambo mengi mengi ambayo tunayajua lakini advantarge yetu tuna timu zuri , wachezaji wetu anauzoefu mkubwa.
"Wanaweza kuvumilia presha lakini advantarge ya pili tunakwenda kucheza bila mashabiki na hiyo itaondoa hofu kwa wachezaji wetu, uwanjani watakuwa wachezaji 11 kwa 11, hakutakuwa na mashabiki kule.Lakini faida ya tatu ni kwamba mechi ya Tunisia ambayo Tanzania itacheza na mashabiki nusu uwanja,"amesema.
Ameongeza na inafahamika Simba ndio timu ambayo kwa Afrika imeongoza kwa kujaza mashabiki wengi uwanja katika michuano ya klabu Bingwa Afrika mwaka 2018."Hapa kwetu mashabiki watakuwepo."
Mo amesema kwa hiyo ameomba kuwatuliwa na wana Simba na watanzania kwa ujumla kwamba wao kama viongozi hawalali wanafanya kazi usiku na mchana ili wakae kwenye reli, wakae kwenye shabaha yao ya kutetea ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya vizuri michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Amesisitiza kwamba wamejipanga vizuri kuelekea michuano hiyo na katika kuhakikisha wanafanya vizuri na kuhusu bajeti kuhusu michuano hiyo amesema wameweka kila kitu sawa na hakuna ambacho kitaharibika, hivyo wana Simba waendelee kuunga mkono klabu yao ya Simba.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment