Mwenyekiti wa Bodi ya Kingdom Leadership Institute, Dkt. Frederick Ringo akizungumza kwenye uzinduzi wa mkutano wa Leadership Summit 2020 uliondaliwa na Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) kushirikiana na Chuo Kikuu cha Regent cha Marekani ambao utatoa kozi ya wiki 14 kuhusu mafunzo ya biashara, uongozi na ujasiriamali ili kujua maadali ya uongozi kwenye biashara. Pia uliunganisha ushirikiano baina ya KLNT na Chuo Kikuu cha Regent cha Marekani na kuunda KLI-REGENT Business Development Centre wenye kauli mbiu ya "Nurturing Leaders as World Changers"
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Regent nchini Marekani, Jason Benedict (kushoto) akisaini mkataba wa ushirikiano baina ya KLNT na Chuo Kikuu cha Regent cha Marekani na kuunda KLI-REGENT Business Development Centre wenye kauli mbiu ya "Nurturing Leaders as World Changers" utalenga kuwajenga viongozi kuleta mabadiliko chanja ya uongozi ulimwenguni. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara, Godwill Wanga (katikati) na Afisa Mkurugenzi Mkuu na Muanzilishi wa KLNT, Isaac Mpatwa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara, Godwill Wanga akizungumza kwenye uzinduzi wa mkutano wa Leadership Summit 2020 uliondaliwa na Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) kushirikiana na Chuo Kikuu cha Regent cha Marekani ambao utatoa kozi ya wiki 14 kuhusu mafunzo ya biashara, uongozi na ujasiriamali ili kujua maadali ya uongozi kwenye biashara
====== ======= ===========
Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) na Chuo Kikuu cha Regent chenye makazi yake Virginia nchini Marekani wametangaza ushirikiano wao rasmi wa KLI-REGENT ambapo kwa pamoja wameunda Kituo Cha Mafunzo ya Biashara nchini Tanzania inayofahamika kama, Business Development Centre. Kituo hiki kitaendesha Mafunzo ya Biashara-Uongozi na Ujasiriamali Nchini Tanzania katika kozi ya wiki 14 jijini Dar es Salaam itakayofanyika hoteli ya Hyatt kuanzia tarehe 14 Novemba. .
Uzinduzi huu mpya wa KLI-REGENT Business Development Centre ulitangazwa rasmi kwenye mkutano wa siku 3 uliokuwa na dhima iitwayo; "Nurturing Leaders as World Changers" ikilenga kuwajengea viongozi uwezo wa kuleta mabadiliko chanya ulimwenguni. Mkutano huu ulihudhuriwa na viongozi 300 wakiwemo wakurugenzi wakuu, wajasiriamali, wafanyabiashara, wakurugenzi wa mashirika, wakuu wa taasisi zisizo za kiserikali, na taasisi za dini ili kujifunza, kutoa uzoefu wa uongozi, na majadiliano baina ya wadau hao juu ya mustakabali wa Tanzania. Mkutano huu ulitoa fursa adimu na kubwa katika kuwakutanisha viongozi, wazungumzaji na watu wenye Mchango mkubwa katika kubadili Maisha ya wengine.
Akizungumza katika mkutano huo, Afisa Mkurugenzi Mkuu na Muanzilishi wa KLNT, Isaac Mpatwa alikaririwa akisema, ‘Business Development Centre nchini Tanzania kinadhaminiwa na Kingdom Leadership Institute (KLI) na Chuo Kikuu cha Regent, Marekani. KLI ni taasisi yenye uweledi katika kutoa mafunzo kwa taasisi zingine katika kusaidia na kuongeza thamani ya uongozi katika maadili ya Kitanzania na Afrika nzima. KLI ipo ili kuandaa viongozi bora zaidi kwa njia ya mwongozo wa maadili, ushauri, kusimamia na mafunzo bora ya uongozi’.
Isaac Mpatwa aliendelea kufafanua, ‘Business Development Centre (BDC) kupitia kozi hizi za wiki 14 kinatoa nafasi ya kipekee zinazolenga kuwasaidia wajasiriamali katika kuanzisha biashara zao.
Kozi hii itawaongoza wanafunzi wenye dira katika ujasiriamali kuendesha taasisi zao kwa ujasiri, uvumbuzi na utaalamu. BDC inahusisha kozi fupi za siku 2 hadi 3 inayofundisha Usimamizi wa Kiutendaji kwa viongozi, ujuzi wa huduma kwa wateja, mikakati ya huduma kwa wateja kwa viongozi, ukaguzi wa mifumo ya biashara na utambuzi wa vitu muhimu vinavyoleta mafanikio.
BDC inatoa fursa ya kipekee kubadilisha uongozi uletao mabadiliko ya uchumi kwa Tanzania kwa vizazi vya sasa na vijavyo kwa kuwapatia viongozi uwezo wa kushawishi, kuhamasisha na kubadilisha Maisha ya wengine na wakati huo huo kujifunza na kukua katika huo uzoefu’.
Mr Mizengo Peter Pinda Waziri Mkuu Mstaafu alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo ambae pia ni mlezi wa KLNT hakusita kuelezea machache. Alisema, ‘Chuo Kikuu cha Regent cha Virginia Marekani kinashikilia orodha ya vyuo vyenye programu bora zaidi za Shahada za Mtandaoni na kimeorodheshwa kati ya vyuo vikuu bora vya kitaifa U.S News na World Report. Regent itawapa wanafunzi uwezo wa kutumia maarifa na ujuzi wao kwa vitendo, kwa uadilifu, huruma, na kusudi huku kwa upande wa KLNT imefanikiwa katika kuendesha programu kila moja ikiundwa kukuza uadilifu, uongozi wa vitendo unaoongeza thamani, ukuaji wa uchumi wa biashara na Uwekezaji nchini tangu 2013. Kwa hivyo, ushirikiano huu mpya kati ya taasisi hizi mbili unatoa nguvu na hamasa kwa mustakabali mzuri wa nchi yetu pendwa’.
Miongoni wa viongozi na wageni wengine mashuhuri waliohudhuria mkutano huu walikuwemo; Dkt Godwill Wanga – Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara, Angelina Ngalula – Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Prof John E. Mulford Jr. Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Regent Kituo cha Ujasiriamali, Jason Benedict, Mikakati, Chuo Kikuu cha Regent Kituo cha Ujasiriamali na wengine wengi.
Kituo hiki kipya kinatarajiwa kusaidia ukuaji wa Biashara ndogo na za kati kwa kuendesha programu kwa siku 14 itakayosaidia wafanyabiashara kupata ujuzi kwa ajili ya ukuaji wao endelevu. Vijana nchini kote hususani wasio na ajira na wavumbuzi wameaswa kujiunga ili wajiongezee thamani yao katika jamii.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment