Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi mfano wa Hudi ya Shilingi milioni mia moja 100,000,000. Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaitenanga iliyotolewa na Banki ya NBC kwa ajili ya kuchangia mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama kwenye Maadhimisho ya Mashindano NBC Marathon mwaka 2020 yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama yaliyofanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 leo Novemba 22,2020 Jijini Dodoma yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama. Mashinda
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa kwenye maadhimisho ya mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama yaliyofanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvisha Medali mshindi wa kwanza wa mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 kilomita 42 Philipo Kipingu kutoka Uganda baada ya kushinda mashindano hayo yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama. Mashindano hayo yamefanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi fedha taslim mshindi wa kwanza wa mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 kilomita 42 Wanawake Muruki Muruki kutoka Kenya baada ya kushinda mashindano hayo yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama. Mashindano hayo yamefanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
========= ========= ==========
Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake nchini kujitokeza kupima afya zao mapema ili kujua hali zao hatua inayosaidia kupambana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
Mama Samia amesema akiongea wanamichezo walioshiriki mbio za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dodoma Marathon yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma.
“Akinamama mjitokeze kupima afya zenu mapema, msiogope kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi hatua inayosaidia kupambana na saratani hii na kulinda afya za watu wetu” amesema Mama Samia.
Katika mashindano hayo, Makamu wa Rais Mama Samia amewapongeza wanawake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizo hatua inayoonesha ni mwanzo mzuri wa kupambana na saratani ya shingo ya kizazi nchini.
Aidha, Makamu wa Rais Mama Samia amesema mashindano ya NBC Dodoma Marathon yamekuja muda mwafaka hatua inayosaidia wanamichezo kujiandaa vema katika mashindano ya Olimpik yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni 2021 Tokyo nchini Japan pamoja na kuchangisha kiasi cha takriban zaidi ya Sh. milioni 75 ambazo zimeelekezwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar kusaidia mapano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Mama Samia amesema kuwa Serikali ipo mstari wa mbele katika kukuza sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kama alivyoahidi Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kufungua Bunge la 12 hivi karibuni Jijini Dodoma.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema wizara yake imesimama kidete kuhakikisha sekta ya michezo nchini inasonga mbele ambapo kwa mara ya kwanza imetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka 2020/2021 kwa ajili ya kusaidia timu za taifa katika mashindano ya kimataifa.
Dkt. Abbasi amemhakikishia Makamu wa Rais Mama Samia kuwa sekta ya michezo hawatamuangusha katika mambo yote yanayohusu michezo mbalimbali ambapo atafanya pia ziara katika mashirikisho yote ya michezo na vyama vya michezo nchini ili kuhakikisha Serikali na wadau wa michezo wanakuwa na kauli moja ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.
Naye Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaisalege amehakikishia Makamu wa Rais Mama Samia kuwa fedha zilizopatikana kutokana na usajili wa wanariadha wa mbio za NBC Dodoma Marathon zitatumiwa na kufanyiwa kazi iliyokusudiwa ili kuokoa maisha ya wanawake nchini.
Dkt. Mwaisalege amesema fedha hizo zinalenga kutoa elimu ya ugonjwa wa saratani, kufungua vituo 25 na kuandaa wataalamu 100 watakaosaidia wananchi kupima saratani ya mara kwa mara hatua itakayosaidia kuepukana na ugonjwa huo na wakigundulliwa kuwa nao waweze kutibiwa mapema na kupona ili waendelee na shughuli zao za kimaendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw. Theobald Sabi amesema kuwa benki hiyo wameona ni vema mapato yote yanayotokana na usajili wa wanariadha zielekezwe kwenye vita na mapambano kwa ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Bw. Sabi ameongeza kuwa njia zote zinazotumika kwenye mbio za NBC Dodoma marathon zimepimwa na mtaalamu kutoka Shirikisho la Riadha Duniani Oktoba 17, 2020 na kutunukiwa vyeti vya utambuzi na uthibitisho na vipo tayari Dodoma.
Fauka ya hayo, Bw. Sabi amesema benki hiyo imepanga kuendelea kuwa wadhamini wa mbio hizo kwa miaka mitano mfululizo ambazo zinatarajiwa kuwa na mvuto kitaifa, kikanda na kimataifa zinazoshirikisha mbio za kilomita 5, kilomita 10, kilomita 21 na kilomita 42.
Mbio hizo za NBC Marathon zimehusisha wanariadha 3000 wakijumuisha wanariadha kutoka hapa nchini, 19 kutoka nchini Kenya, 12 kutoka Uganda pamoja na wanariadha wanne (04) kutoka Malawi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment