MIRERANI KUPAMBANA NA MBWA VICHAA | Tarimo Blog

 

Ofisa afya wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jovin Rweyemamu akizungumza kwenye kikao kazi cha Mamlaka ya Mji huo.
Wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye kikao kazi cha Mamlaka hiyo.
Mjumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Joyce Mwasha akizungumza kwenye kikao cha Mamlaka hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Evence Mbogo akizungumza kwenye kikao kazi cha Mamlaka hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Christopher Chengula na kulia ni Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani, qqASP Christina Mkonongo.
*******************************************
ILI kupambana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa, wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamejipanga kuhakikisha wanawadhibiti mbwa wote wanaozuruza ovyo kwa kuwapiga risasi.
Ofisa afya wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani, Jovin Rweyemamu akizungumza kwenye kikao cha Mamlaka hiyo alisema hivi karibuni watu wanne wameng’atwa na mbwa wenye kichaa kwenye eneo hilo.
Rweyemamu mbwa wanaozurura ovyo wenye vichaa waliwangata watu wanne ambao walitibiwa kwenye zahanati za mitaani kea sh30,000 kwa kila mmoja. 
Alisema mbwa hao wanaozurura ovyo wanapaswa kuchukuliwa hatua kwani watasababisha vifo kupitia ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
“Uking’atwa na mbwa na usipopata matibabu mapema unapoteza maisha yako hivyo suala hilo lichukuliwe hatua kwa haraka ili madhara yasitokee,” alisema Rweyemamu.
Mwenyekiti wa mtaa wa Endiamtu, Nalogwa Mkumbo alisema mbwa wote wanaozurura ovyo wanapaswa kuchukuliwa hatua na siyo mbwa wenye vichaa pekee.
Mkumbo alisema wao kama viongozi wa wananchi wanapaswa kusimama kidete kuhakikisha wanapambana na tatizo hilo ili lisilete madhara.
Mwenyekiti wa mtaa wa Songambele, Daudi Makala alisema Serikali inapaswa kuchukua hatua kwenye jambo hilo.
Makala alisema kila mfugaji wa mbwa ahakikishe mbwa wake anapata chanjo na kufungiwa kwenye banda.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Adam Kobelo aliwataka wenyeviti wa mitaa ya Mji huo kusimama upande wa Serikali Ili kuhakikisha suala hilo linamalizika.
Kobelo alisema wenyewe hao wanasimamia maeneo yao ipasavyo kwa kuhakikisha mbwa waliopo katika sehemu zao wanapatiwa chanjo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2