Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufanya ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kukagua maduka na magodauni yanayohifadhi simenti katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
**************************************
NA VICTOR MASANGU, PWANI
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amefanya ziara ya kikazi ya siku moja kwa wauzaji wa simenti katika Halmashauri ya mji wa Kibaha kwa ajili ya kuweza kujionea mwenendo mzima na kukagua bei iliyopo kwa sasa ili kuweza kuona namna ya serikali itavyowasaidia wauzaji hao.
Ndikilo akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa alisema, amelazimika kufanya ziara hiyo akidai kuwa alidhani saruji haipatikani hivyo kutembelea kwenye maduka yanayouza bidhaa hiyo
Alisema baada ya kufanya ziara hiyo amebaini tatizo lipo kwenye kuchelewa kwa bidhaa hiyo kufika dukani na hivuo kusababisha kupanda kwa bei.
Katika ziara hiyo baadhi ya maduka yalikutwa hayana saruji kabisa huku mengine yqkiwa na kiasi kidogo wengi wakilalamika foleni iliyopo viwandani.
Mkuu huyo wa mkoa alisema, wauzaji wa saruji wa Mkoa huo wanategemea kupata bidhaa hiyo kutoka kiwanda Cha Dangote, Simba na kemal hivyo foleni inayoelezwa inwezekana kuwa chanzo cha kupanda kwa gharama za uuzaji.
Baadhi ya wauzaji wa bidhaa hiyo katika Halmashauri ya mji wa Kibaha wamelamikia upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa wakati.
Mchicha Mohamed alisema kwasasa anauza saruji kwa Sh. 15000 awali ilikuwa sh 14,000 huku akinunua kwa Shilingi 13,500.
Mchicha alimueleza mkuu wa Mkoa kuwa kwasasa upatikanaji wa Saruji umekuwa wa shida madereva kukaa kwa muda mrefu foleni ya kusubiri mzigo.
Naye Adam Mwasha alisema, tangu Novemba 15 hadi sasa hana saruji ya kuuza kutokana na foleni iliyopo katika kiwanda cha Simba huko Tanga.
Halfan Mwembamba alisema kwasasa upatikanaji wa Saruji imekua kikwazo kwao kufanya biashara vizuri pamoja na mabati ambayo nayo yameanza kuwa adimu.
Afisa Masoko wa Wakala wa usqmbqzaji wa Saruji ya Kampuni ya Twiga Denis Madege alisema kiwanda chao kinaendelea na Uzalishaji lakini kutokana na mahitaji kuwa makubwa upatikanaji wake umekuwa kikwazo.
Madege alisema, wapo watu wamelipia tani 300 za Saruji lakini hadi sasa hawajafanikiwa kukamilisha oda hiyo kutokana na foleni iliyopo kiwandani.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment