Redio Jamii zilivyobadilisha jamii Zanzibar | Tarimo Blog

UWEPO wa redio jamii umechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko yaliyotokea katika jamii kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Redio jamii ambazo zinaendeshwa katika jamii husika kwa kutumia waandishi wa habari wa jamii hizo, zimekuwa zikitoa elimu kubwa inayohamasisha wana jamii kuchukua hatua ili kujikomboa kiuchumi na kisiasa pia kupinga masuala ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto. 

Mkurugenzi wa redio jamii Tumbatu, Haji Adam Haji ambayo iko Mkoa wa kaskazini Unguja katika kisiwa hicho cha Tumbatu, alisema awali wanawake wa kisiwa cha Tumbatu walikuwa hawajishughulishi na shughuli za vipato na hawakuwa kabisa wakiripoti matokeo ya kiudhalilishaji wakiamini kuwa ni mwiko.

Mkurugenzi huyo alisema redio hiyo ilioanzishwa mwaka 2014, imechukua juhudi za kuwahamasisha wanawake wajiunge kwenye vikundi, kupata elimu ya upigaji kura pamoja na kuripoti masuala ya kiudhaliliaji yakiwemo kupigwa na kubakwa.

Alisema hivi sasa hali ya usiri mkubwa imeondoka na kwamba kesi hizo za ubakaji, kukashifu, kupigwa na kutelekeza zimekuwa zikiripotiwa.

Alisema kwa mfano mwaka 2019 kesi zaidi ya 31 zimeripotiwa polisi ambapo kituo chake kilishiriki katika kufuatilia katika ngazi mbali mbali zikwemo kwenye jamii.

Alisema kuwa awali wanawake wengi walikuwa wakipiga kura kwa mujibu wa matakwa ya waume zao ama jamaa zao lakini baada ya kupata elimu ya wapiga kura wanawake hao wameelewa kuwa kura ni haki yao wao kuamua nani wampigie.

Alieleza pia kuwa kituo chake kimekuwa kikifuatilia uundwaji na ukuwaji wa vikundi 12 vya wanawake ambavyo vinajihusisha na biashara mbali mbal ikiwemo vya urembo, ushoni na ufugaji.

Alisema kwa kipindi chote hicho kituo chake kimekuwa kikisaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mafunzo na vifaa.

Alisema miongoni mwa jambo ambalo anakumbuika kabla ya kuanzishwa kwa redio hio ilikua ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi kuzikimbia ndoa zao bila kutoa huduma na kuenda maeneo mbali mbali kwa ajili ya shughuli za uvuvi ambapo wengine hukaa huko kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Alisema kutokana na mazingira hayo familia nyingi zilikosa huduma na wengi wao walijikuta wanaingia kwenye dimbwi la umasikini mkubwa na wakati mwengine kusababisha watoto kuacha kwenda shuleni.

Kwa upande wake Mhariri mkuu wa redio hio Juma Haji Juma alisema kupitia vipindi mbali mbali vya redioni hapo imekua sababu kuu kujengwa kwa kituo kujifungulia wazazi ndani ya kisiwa hicho.

Alisema kabla ya kujengwa kituo hichio cha afya wapo akinamama wengi waliojifungua nyumbani na wengine hata kwenye usafiri wa boti wakati wakifata huduma za kujifungua nje ya kisiwa hicho na kwa masikitiko makubwa wapo waliopoteza maisha.

Hata hivyo alisema licha ya uwepo wa mafanikio makubwa lakini pia wamekua wakikabiliwa na changamoto ikiwemo ukosefu wa usafiri wa uhakika wa boti ambao ungewaweza kuvuuka kwa wakati na kufuata taarifa nje ya kisiwa hichio.

Alisema kwa kuwa redio yao inasikika maeneo mengi ya mkoa wa kusini Unguja walipaswa kufanyia kazi taarifa mbali mbali ambazo zinatokea nje ya Tumbatu lakini wamekua wakishindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa usafiri wa boti ya uhakika.

Baadhi ya wanajamii ambao ni waskilizaji wa redio hio walisema kuna mabadiliko makuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho.

Miongoni mwa wanajamii hao ni Mzee Makame Mcha ambaye alisema licha ya kazi mbali mbali zilizoendelea kufanywa na redio hio lakini pia imekua ikitoa taarifa muhimu zinazowahusu walengwa wenyewe.

Alisema wananchi wengi wameelewa masuala ya umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari, umuhimu wa kusomesha watoto skuli, kuelewa haki za msingi na kupinga vita masuala ya ukatili wa kijinsia.

Wakati hayo yakijiri kwa redio Tumbatu ilipo kaskazini mwa kisiwa cha Unguja inaelezwa kuwa hali yenye kufanana na hio pi ipo kwa redio jamii Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba. 

Mkurugenzi wa redio hio Ally Masoud anasema 2009 kwa lengo maalumu ambalo kwa kiasi kikubwa limefanikiwa.

Akitaja miongoni mwa kampeni ambazo walianza kupambana nazo ni pamoja na uwepo wa njaa kali kwa wananchiu wa eneo hilo kwa kuwa wengi wao hawakua wakijikita na kilimo kufuatia ardhi yao kutokua rafiki.

‘’Wananchi wengi walikua hawajui kilimo mbadala kwa kuwa ardhi yetu ni ya mawe walipaswa kuwa na mbinu nyengine na ndio tulizokwenda kuwafundishana sihaba tumefanikiwa’’aliongezea.

Kaimu,Meneja wa radio Mkoani, Said Omar Said akiwekea mkazo suala la kilimo alisema kituo chake kimeweza kuwahamasisha wanawake wa mabonde ya mpunga makubwa yaliyoko Mkoani ya Mjimbini,Kiwani and Makombeni kutumia kilimo cha umwagiliaji maji.

Alisema kituo kiliweza kufanya pia mazungumzo na wadau mbali mabli jinsi ya kuwasaidia wananchi hao ambapo sasahivi tayari wameweza kufungiwa vifaa vya umwagiliaji maji.

Alisema pia redio imekuwa mstari wa mbele kushajihisha watoto wapelekwe skuli na kufichua ukaitli wa kijinsia ambapo kwa miaka mingi wananchi wanaona ni mwiko kuyazungumzia na hivyo kufanyiwa bila ya kutolewa adhabu yoyote.

“Hadi sasa bado kuna vijiji ambavyo havitaki kuripoti kesi hizo lakini huwa tunavifatilia kwa karibu ili kutokomeza vitendo hivyo viovu”, alisema.

Alisema pia vijiji vyengine hadi leo watoto hasa wa kike hawapelekwi shule kabisa jambo ambalo linahitaji kurekebishwa na kwamba kituo kitaendelea kubadilisha mawazo ya wanajamii hao.

Mmoja miongoni mwa wazazi kutoka Mkoani, Bi Mize Mohammed alisema kabla ya uwepo wa redio hio hakuelewa sana umuhimu wa elimu.

Alieleza kuw akila asubuhi alikua akiwaamsha watoto wake watoke na kwenda kuuza bidhaa bandarini Mkoani ili waweze kupata pesa za kusaidia maisha yao.
"Lazima tuseme ukweli uwepo wa redio hii umechangia mabadiliko makubwa kwenye jamii yetu maana watoto wengi awali walikua hawaendi na wengine hata kutoandikishwa skuli.’’aliongezea.

Mkurugezi TAMWA Zanzibar Dkt.Mzuri Issa Ally aliendesha mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo wafanyakazi wa redio jamii Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2