Mwandishi wetu, DODOMA
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ndugu Andrew Massawe, amesema matumizi ya vifaa vya kisasa ambavyo OSHA imewekeza, itasaidia sana kupunguza malalamiko sehemu za kazi, kutokana na kuwa na majibu yenye uhakika Zaidi.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili , yaliyoandaliwa na OSHA maalamu kwa wakaguzi wa Afya toka OSHA, yaliyofanyika jijini Dodoma, Massawe amesema matumizi ya vifaa vipya vya kisasa hususani kipimo hiki cha macho ambavyo taasisi hiyo imewekeza itasaidia sana kupunguza malalamiko ya baadhi ya wafanyakazi, kutokubaliana na majibu ya vipimo ambavyo wanapatiwa, na vile vile itasaidia kuwafikia watu wengi.
“kitendo cha taasisi hiyo kuwekeza kwenye vifaa vya kisasasa ni jambo la kupongezwa na ni jambo zuri, amesema taasisi hivyo kuwa na vifaa hivyo vya kisasa ambavyo ni maalumu kwaajili ya kupima uwezo wa macho kuona, aidha Katibu Mkuu huyo amewataka OSHA kuangalia namna pia ya kupata vifaa vya vingine vya kisasa kwenye maeneo mengine”alifafanua ndugu Andrew Massawe.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema lengo la mafunzo hayo ni sehemu ya program ya taasisi hiyo kuwajengea uwezo Zaidi wakaguzi wa Afya wa OSHA, na mafunzo ya leo yalikuwa maalumu juu ya matumizi ya vifaa vipya vya kupima macho ambavyo taasisi hiyo imenununua.
Bi.Mwenda amesema vifaa hivyo vya macho ambavyo kitaalamu vinajulikana kama VT 1 master ambacho taasisi hiyo imenunua ni vya kisasa Zaidi, na vina wigo mpana Zaidi wa kutoa majibu tofauti na kifaa cha snell chart ambacho chenyewe kina uwezo wa kupima uwezo wa macho kuona mbali au karibu tu, hivyo kushindwa kubainisha changamoto zingine za macho zinazomkabili mtu, kama vile kushindwa kutofautisha rangi, kuona usiku.
“ Kazi yetu pia ni kufanya uchunguzi wa ajali sehemu za kazi zinapotokea,tathimini ndogo tulioifanya, tuliona kuwa ajali nyingi zinazotokea sehemu za kazi, ukiwauliza wahusika wanakuambia hakuona kilichotokea, tukaona kwamba kumbe mtu anaweza akawa na matatizo ya macho bila yeye kujua na hivyo kusababisha ajali. ”
Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dr Robert Mazengo amesema vifaa hivyo vya kupima macho ambavyo OSHA, imevipata ni vifaa vya kisasa zaidi, na vinauwezo mkubwa zaidi wa kubaina mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuwashauri waajiri zaidi.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo kutoka OSHA Bi Amina Nangu na Daktari Rajabu Mambo, wamesema, wao kama wakaguzi matumizi ya vifaa hivyo kwa vitakuwa msaada sana, kwani vitasaidia kutoa majibu yenye uhakika Zaidi na vitaokoa muda kwani, kifaa hicho kinauwezo wa kupima watu wengi Zaidi kwa wakati mmoja, tofauti na kifaa cha zamani ambacho ni Snells Chart.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment