Na Pamela Mollel Michuzi TV,Mererani
Wamiliki wa migodi ya Madini ya Tanzanite iliyopo ,Mererani wilayani Simanjiro ,Mkoani Manyara wameipongeza Serikali kwa hatua ya kufunga mfumo wa CCTV kamera zipatazo 306 kuzunguka ukuta jambo litakalosaidia kuiweka salama migodi yao na kupunguza wizi mdogo mdogo.
Aidha wameiomba serikali kusaidia kupunguza kodi kwa vifaa vya uchimbaji ili waweze kuvipata kwa gharama nafuu tofauti na sasa ambapo wanauziwa kwa gharama kubwa
Kauli hiyo wameitoa katika ziara ya Katibu mkuu wa Wizara ya Madini na viongozi mbalimbali walipotembelea baadhi ya migodi ya wachimbaji hao na kusikiliza kero zao katika hafla ya serikali kukabidhiwa kwa mradi wa CCTV Kamera 306 zilizofungwa kuzunguka migodi hiyo hivi karibuni
Wakiongea kwa nyakati tofauti wamikiki hao wa migodi akiwemo bilionea Saniniu Laizer na mzee Said Nasoro walimpongera rais John Magufuli kwa hatua ya ujenzi wa ukuta na ufungaji wa kamera wakisema itasaidia kulinda rasilimali za madini zilizopo katika migodi hiyo.
"Hatua ya Rais Magufuli kufunga Kamera kuzunguka migodi yetu ni jambo jema sana kwani itasaidia sana kupunguza wizi na migodi itabaki salama " alisema Laizer
Katika hatua nyingine Laizer alimpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili kuwa Rais wa Tanzania akidai kuwa ndiye tegemeo la watanzania katika kuinua uchumi wa Taifa hilo.
Naye meneja wa mgodi wa Deogratias Minja (Calfonia Camp), Omari Mandali
amesema wamefarijika kuona viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwatembelea katika mgodi wao na kujua kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitatua, suala ambalo limewapa faraja ya kulipa kodi ya serikali vizuri .
"Tangu ukuta huu umejengwa kuzunguka Migodi yetu tumekuwa salama sana na uchimbaji umekuwa Mzuri sana na kodi ya Serikali tunalipa vizuri sana" alisema Mandali
Naye Mkurugenzi katika Mgodi wa Saidi Nasoro,Iddy Kondo alisema kuwa Ujenzi wa ukuta na ufungaji wa mfumo wa CCTV Kamera umewasaidia sana katika ulinzi wa migodi yao kwani hata kama Madini yakipatikana bila mmiliki wa Mgodi kuwepo wana uhakika wa kuyakuta Madini hayo salama.
"Kwa sasa Serikali imeonyesha ipo kazini awali haya Madini yalikuwa hayana mwenyewe watu walikuwa wanapata hasara ,wawekezaji walikuwa hawaji kwa sababu ya usalama ila kwa sasa tunaishukuru sana Serikali kwa kutuimarishia Usalama katika migodi yetu" Alisema Kondo
Meneja wa mgodi wa Saidi Nasoro,Adam Jastin akitoa maelezo ya mgodi kwa timu ya katibu Mkuu Wizara ya madini walipotembelea baadhi ya migodi Mererani,kushoto ni katibu Mkuu Wizara ya Uliñzi Dkt Faraji Kasidi
Picha ya pamoja Mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya madini Profesa Simon Msanjila na viongozi wengine kutembelea mgodi wa Calfonia Camp hivi karibuni
Jiko maalumu la kuchomea Nyama katika mgodi wa Said Nasoro lilikuwa kivutio kikubwa kwa wageni waliofika katika mgodi huo
Wageni mbalimbali wakishangaa jiko maalumu la kuchomea nyama
Bilionea Saniniu Laizer akizungumza na waandishi wa habari kupongeza Serikali kwa hatua ya kufunga kamera katika ukuta wa Mererani
Muonekano wa kamera hizo zinavyochukua matukio mbalimbali katika eneo hilo la migodi
Mkurugenzi wa mgodi wa Said Nasoro,Iddy Kondo anasema Serikali ipo kazi kwa kazi kubwa inayofanya ya kuhakikisha wachimbaji wanakuwa salama.
Mkurugenzi wa mgodi wa Said Nasoro,Bwa.Said Nasoro akiongea na vyombo vya habari huku akipongeza Serikali kwa hatua kubwa ya kufunga kamera katika ukuta huo
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment