Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Profesa Mabulla Nchembe amesema kwamba kuzaliwa njiti na uzito pungufu ni tatizo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuongezaa vifo vya watoto wachanga hapa duniani na kwamba kiasi cha watoto milioni 15 kila mwaka huzaliwa wakiwa njiti.
Profae Nchembe amesema hivyo tatizo hilo ni kubwa na linasababisha watoto wengi kufariki kwasababu watoto wachanga hawawezi kutunza joto mwilini na sababu nyingine zinazochangia vifo vya watoto wachanga njiti ni pamoja na mtoto kushindwa kupumua, maambukizi ya bakteria na mtoto mchanga kuzaliwa na kasoro za viuongo vyake mwilini.
Amesema hayo jana Novemba 17, 2020 alipokuwa akizungumza kwenye siku ya Maadhimisho ya Mtoto Njiti Duniani ambapo kwa Tanzania, Taasisi ya Doris Mollel Foundation chini ya Mwanzilishi na Mkurugenzi wake Doris Mollel.Katika kuadhimisha siku hiyo taasisi hiyo iliamua kuandaa tukio la kuwasha taa za rangi zambarau kama ishara ya kuonesha upendo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Akizungumza zaidi wakati Maadhimisho hayo, kwa niaba ya . amesema Wizara inafurahishwa na kinachofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation na kwamba leo ni siku kubwa kuadhimisha siku ya mtoto njiti duniani.
"Niko hapa kwa ajili kumuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Nchembe lakini anachosema ni kwamba angefurahi sana siku ya angekuwa hapa.Kabla sijasema ya katibu mkuu kwasababu kwa itifaki natakiwa kuyasoma kama yalivyoandikwa,"amesema.
Akifafanua zaidi kwa niaba ya Katibu Mkuu, Profesa Andrew Barnabas Pembe amesema vifo vya watoto wachanga bado ni tatizo kubwa nchini , kwa mujibu wa takwimu za afya nchini za 2015/2016 vifo hivyo vinachangia asilimia 40 ya vifo vyote vya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.
Aidha takwimu zinaonesha kati ya watoto 1000 wanaozaliwa watoto 20 hupoteza maisha kabla ya siku 28, taarifa za wizara zinaonesha mwaka 2019 jumla ya vifo vya watoto wachanga 11524 vilitokea nchini.Takwimu zinaonesha watoto wachanga 25 kati ya 100 ambao wanafariki hufariki kutokana na matatizo yanayoambatana na kuzaliwa na uzito pungufu na wengi wao ni watoto walio njiti.
"Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati ni pale ambapo mtoto huzaliwa kabla ya mimba haijakamilisha wiki 37 za ujauzito yaani mimba kukomaa.Hapa nchini tatizo hili ni kubwa taarifa ya mwaka 2012 inaoneshaTanzania ni kati ya nchi 20 duniani zinazoongoza kwa kuzaliwa watoto njiti ambazo zinafikia jumla watoto 2,130, 000 kwa mwaka watoto njiti huwa katika hatari zaidi ya kupoteza maisha ukilinganisha na watoto wanaozaliwa ambao wanazaliwa baada ya kumakamilisha wiki 37.
"Takwimu zinaonesha watoto njiti wako kwenye hatari hiyo mara sita hadi 26 ukilinganisha na watoto ambao wamekomaa, sio tu hatari ya kufa lakini watoto njiti wako katika hatari ya kupatwa na vilema mbalimbali kama vile matatizo ya kuona na kusikia , matatizo ya mapafu na matatizo ya moyo, "amesema.
Profesa Pembe amesema kuna sababu zinazosababisha mtoto kuzaliwa njiti, sababu hizo ni pamoja na historia ya kuzaa njiti, umri ya mama mjazito kuwa mdogo, mjamzito kufanya kazi zito, wakati wa ujauzito bila kupumzika, mimba za kukabiliana sana, lishe duni, upungufu wa damu na shinikizo la damu.
"Ili kutatua changamoto ya watoto njiti na matatizo ya watoto hao kwa ujumla Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kuboresha huduma za kliniki kwa mama mjazito na huduma kwa mtoto mchanga aliyezaliwa njiti.Baadhi ya hatua zinazochukuliwa ni kuwapatia dawa wajawazito ambao wanaonekana kujifungua njiti.
"Mengine ni kuimarisha huduma ya mama kangaroo katika ngazi ya hospitali na vituo vya afya inayotolewa na mama kumsaidia mtoto kutunza joto la mtoto njiti.Watoto njiti na watoto wachanga kwa ujumla wanaweza kufa kutokana na kushindwa kuzalisha na kutunza joto la kutosha,pia kuanzishwa kwa vyumba maalum kwa ajili ya matibabu ya watoto wachanga,wagonjwa kwenye baadhi ya hospitali, hospitali 104 kati ya hospitali 340 zinatoa huduma hiyo,"amesema.
Pia kuwajengea uwezo watoa huduma watoe huduma bora zaidi, kuongeza ununuzi wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matibabu ya watoto wachanga wagonjwa pamoja na kuanzisha miongozo mbalimbali inayoweza kuboresha huduma ya afya ya uzazi na mtoto njiti.
Ametoa rai katika kuboresha afya ya mjazito ni vema kuhakikisha wanahudhuria kliniki na kupata huduma, kuhakikisha akina mama wote wanajifungulia kwenye vituo vya kutoa huduma, na vile vile kuhakikisha wanahudhuria kliniki baada ya kujifungua, akiwemo mama mwenyewe pamoja na mtoto wake mchanga.
Amezungumzia umuhimu wa kuongeza nguvu kuchagiza halmashauri zote katika kuongeza vyombo vya matibabu kwa watoto wachanga, jamii ihamasike na kufahamu lishe bora ambayo hupunguzia kazi mama mjazito kwani ni miongoni mwa mambo muhimu katika kupunguza mama mjazito kuzaa njiti.
Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amesema anaungana na wazungumzaji waliotangalia kumpongeza Doris kama Doris kwani kwa muda mrefu amekuwa balozi mzuri wa kuendelea kustawisha afya na akijikita zaidi kwa mtoto njiti.
"Na mimi nimefahamu Doris akiwa mdogo naye alikuwa njiti , lakini siiamini kama anafanya hivi kwasababu naye alikuwa njiti, bali anafanya kwasababu ya moyo mzuri mwema ambao Mungu amempa wa kusaidia watu wengine wenye uhitaji.Nimekuja kwasababu ya kumuunga mkono Doris lakini katika Chama Cha Mapinduzi mimi ni msimamizi wa sera.
"Na leo nimejifunza na nimechukua yote, niseme mambo mambo machache tu kwamba Chama kimeeleza kwa serikali kwamba hospitali zote zinazojengwa katika halmashauri zaidi ya 100 tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, zitakuwa zinatoa huduma kuhakikisha watoto waliozaliwa kabla ya wakati, wenye uzito mdogo wakiemo njiti wanapata huduma stahili.
"Ili kuhakikisha na wao wanafurahia haki ya maisha na kuishi kama wengine na hiyo itakwenda sambamba na vyumba maalum vyenye joto ambalo watoto njiti wanalihitaji wakati wote lakini na vifaa vingine tiba ambavyo vinahitajika wakati wote.
"Chama kimeamua na tayari kinafanyia kazi, na Serikali hivi karibuni tumeielekeza iweke utaratibu wa kuhakikisha ya watu wote wanakuwa na bima ya afya kwa ajili ya kupata matibabu ili wakati wowote mtu akiumwa asipate changamoto ya kukosa matibabu.
"Hivyo tayari hilo limeelezwa na Bunge limeshapewa maelekezo ili watanzania wote wawe a bima ya afya kwa gharama ambayo wanaweza kuimudu , na mimi nimeguswa sana na mdau , kutetea haki, ujinsia na wanawake kwamba jambo la malezi la watoto njiti wakiwa wadogo liwe la jinsia zote kwa maana na baba nao washriki katika kwenye kangaroo,"amesema Polepole.
Wakati huo huo Doris ametumia nafasi hiyo kueleza katika jitihada za kuhakikisha watoto njiti wanakuwa salama wamepeleka maombi Serikalini na baadhi ya maombi hayo ni kuwa na likizo maalum ya uzazi kwa mama wanajifungua watoto njiti, kwani wanahitaji muda wa kutosha kuangalia watoto.Pia wameomba kuanzishwa kwa silabasi shuleni ambazo zitafundisha masuala ya watoto njiti.
Makamu Mkuu wa Chuo Kiku cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Profesa Andrew Barnabas Pembe kwa niaba ya Katibu Mkuu Profesa Nchembe akizungumza kuhusu namna Serikali kupitia wizara ya Afya wanavyoshirikiana na Taasisi ya Doris Mollel ili kuweza kuokoa watoto wanaozaliwa kabla ya muda wakati wa maadhimisho Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi na Mhasisi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akitoa shukrani kwa wadau mbalimbali wanaosaidia taasisi hiyo kuweza kuwafikia watoto Njiti ili kuweza kukua vizuri wakati wa maadhimisho Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akizungumza kuhusu namna Chama hicho kinavyochukua maoni ya wadau mbalimbali yakiwemo ya Doris Mollel Foundation ili kuja na majibu yatakayoleta maendeleao kwa jamii nzima wakati wa maadhimisho Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es SalaamMkurugenzi wa Uuguzi wa Muhimbili Sist. Zuhura Mawona akizungumzia namna uongozi wa Hosptali ya Taifa ya Muhimbili inavyoshirikiana kwa karibu na Doris Mollel Foundation ili kuweza kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na kupewa huduma katika hospitali hiyo wakati wa maadhimisho Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Programu za Vijana Shirika la Childbirth Survival International(CSI) CSI, Ester Mpanda akizungumza kuhusu CSI inavyoshirikiana na Doris Mollel Foundation wakati wa maadhimisho Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam
Mgeni rasmi Makamu Mkuu wa Chuo Kiku cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Profesa Andrew Barnabas Pembe pamoja na Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioiwezesha taasisi ya Doris Mollel kuweza kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi na Mhasisi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taasisi hiyo ilivyoweza kuandaa sherehe maalum kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwenye wa maadhimisho Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment