Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya Wakurugenzi na Mameneja wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi nchini kupitia Chama chao cha TAMASCA kuendelea kutunza heshima ya makampuni hayo na kufuata misingi ya vibali vinavyowaongoza ikiwa ni pamoja na sheria za nchi.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa siku moja wa Chama cha Makampuni ya Ulinzi Watu Tanzania TAMASCA uliofanyika jijini Dodoma, wenye lengo la kufanya tathimini na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake hadi sasa.
Akisoma risala mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Bwana Shawiniaufoo Kimuto, amesema kuwa, licha ya Makampuni binafsi ya ulinzi kuendelea kufanyakazi kwa uzalendo lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ikiwemo mafunzo ya weledi na umilikishwaji wa silaha.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment