JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA KULA SAHANI MOJA NA MADEREVA WAZEMBE | Tarimo Blog


Mrakibu wa Jeshi la Polisi,Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma Kikosi cha Usalama Barabarani Mossi Ndozero akizungumza na madereva wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi ya Mkoani kuhusiana na operesheni na utoaji wa elimu kwa madereva na Abiria katika kituo hicho,Jijini Dar es Salaam.
Mrakibu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma Makao Makuu ya Kikosi cha Polisi Cha Usalama Barabarani Makao Makuu Mossi Ndozero akizungumza na Abiria na Basi linalofanya safari kutoka Dar es Salaam namna ya kufanya mawasiliano kati ya Dereva na Abiria katika kuhakikisha safari inakuwa salama.
Baadhi ya madereva na makondakta wakisikiliza maelezo ya Afande Ndozero hayupo pichani.
Afande SP Ndozero akipata maelezo kutoka kwa Askari wakati wa operesheni katika kituo cha Mabasi Ubungo, Jijini Dar es Salaam.
Afande Ndozero akimsikiliza maelezo ya operesheni katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo Jijini Dar es Salaam.

 


*Afande Ndozero asisitiza abiria kupaza sauti pale wanapoona changamoto 

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama wa Barabarani Kimesema kuwa hakitaki madereva wazembe wakati wakisafirisha abiria kwa kipindi chote.

Jeshi hilo licha ya kutaka madereva kuwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na upande wa abiria wanatakiwa kupaza sauti pale wanapoona dereva anahatarisha maisha yao kwa kupiga simu makao makuu ya Jeshi hilo Kikosi cha Usalama Barabarani.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu kwa abiria na madereva Mrakibu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa  Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Mossi  Ndozero  amesema kuwa madereva wanaokiuka sheria hawatavumiliwa kwa kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa kufuata sheria za usalama barabarani.

Mrakibu huyo amesema kuwa katika kipindi hiki madereva wamekuwa wakitumia njia ya kuongeza viti ambavyo ni madumu na mito katikati ya viti na viti.

Aidha amesema kuwa wananchi wahakikishe wanasafiri kwa nauli iliyopo kwa mujibu wa sheria kwa kuambizana kati ya abiria na abiria.

"Jeshi la Polisi tumejipanga pamoja na kufanya operesheni kwa kila siku kwa madereva wa mikoani pamoja na usafiri wa ndani ya miji kwa kuamini kuwa ajali za uzembe wa watu hazipatiwi nafasi"Amesema Afende Mosi

Jeshi hilo pia Kimesema kwa kipindi hiki cha sikukuu kwa madereva kuacha mazoea kwenda mwendo wa Kasi kwani kitengo cha taa kiko imara.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2