Hatua hiyo inatajwa kuifunga milango kwa mpinzani wake Donald Trump, katika jitihada zake za kisheria za kuyageuza matokeo ya uchaguzi wa 2020. Hatu hiyo inafanyika huku mteule huyo akimkosoa mpinzani wake huyo kwa maneno makali tangu kumalizika kwa uchaguzi kwa kumwita mpinga matakwa ya umma na mkaidi katiba ya nchi.
Wakati Biden akipiga kampeni ya kuunganisha taifa, baada ya uchaguzi uliowagawa Wamerekani, wajumbe kutoka majimbo yote jana Jumatatu, kwa matokeo stahiki ya kura za wajumbe zinazohitajika 270. Hatua hiyo maana yake ni kumsafishia njia sasa kuekea kuingia katika ofisi za Ikulu ya Marekani Januari 20.
Hatma ya Urais wa Marekani, kwa Trump itasalia kuwa ndoto
Kimsingi Biden alifikia hatua ya uhakika wa ushindi baada ya nyongeza ya kura 55 za jimbo la California. Na pia baada ya Hawaii kumfanya kuongeza idadi ya kufikia jumla ya kura 306. Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump alipata 232.
Utaratibu wa kura za wajumbe, ambao umedumu kwa takribani miaka 200, umepiga msumari wa mwisho kwa kusema matakwa ya umma yamezingatiwa pamoja na kutokea purukushani za hapa na pale. Na Trump kukataa kukubali kushindwa. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment