Maendelea ya nchi yanahitaji kuzalisha wasomi wa kutosha-Katibu Mkuu Doto James | Tarimo Blog

*Profesa Nombo ajivunia mafanikio ya TIA katika uzalishaji rasilimali yenye utaalam.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

 SERIKALI imesema kuwa nchi yeyote ili iweze kuendelea inahitaji wasomi na bila kufanya hivyo hatutaweza kuzifikia nchi zilizoendelea katika karne ya sasa.

Hayo ameyasema Karibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James wakati wa mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) kwa Kampas ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika Kampas ya Dar es Salaam.

James amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kwenda kufanyia kazi elimu yao kwa uadilifu,Weledi, Ubunifu, pamoja na kujiepusha na rushwa.

Amesema kuwa  TIA iko chini ya wizara Fedha na Mipango hivyo hawahitaji wafanyakazi wazembe na wasio wabunifu kutokana na kuamini Taasisi hiyo inapika rasilimali yenye sifa zote za kufanya Fedha na Mipango inakwenda kutatua changamoto za watanzania.

James amesema Wizara itaendelea kuwa karibu na Taasisi katika kuweza kwenda kasi katika Mipango yake ujenzi wa vyuo kwenye mikoa Kigoma Pamoja Mwanza ndani ya miaka miwili viwe vimeshakamilika.

Aidha amesema kuwa wahitimu watumie taaluma hizo pamoja na kujiajiri kutokana na changamoto ya ajira ambayo haiko Tanzania tu ni suala la dunia nzima.

"Tunaamini wahitimu watatumia taaluma zao katika kuleta Maendeleo ya nchi na kuweza kuzifikia nchi zilizoendelea ambazo zilianza kuwekeza katika kuandaa wataalam mbalimbali"amesema James.

Amesema soko la ajira rasmi ni dogo sana ambalo halikidhi mahitaji ya wahitimu wote nchini hivyo kunahitaji kwenu kuendeleza mawazo kwenye kujiajiri badala ya kusubiri ajira za kuajiriwa.

"Vishawishi vya vitendo vya  rushwa, ubadhirifu na vinginevyo visivyo halali vina madhara makubwa kwa maisha ya mtu mmojammoja na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla."Amesema James.

Nae Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa Carolyne Nombo amesema kuwa wamewaanda wahitimu kwa kuzingatia soko la ajira ambao wanaweza kujiajiri au kuajiriwa na kufanya vizuri katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Profesa Nombo amesema kuwa kwa Kampas ya Dar es Salaam na Mtwara wanafunzi 5,545 wamehitimu katika mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada za uzamivu.

Amesema katika mahafali hayo Taasisi imeweza kupiga hatua mbalimbali ya maendeleo kupitia mafunzo ,huduma za Utafiti na ushauri, Ustawi wa Wafanyakazi Pamoja na miundombinu ya kusomea na jufundishia na kufanya fursa kuongeza udahili hadi kufikia wanachuo 10,871 kwa mwaka 2020/2021.

Profesa Nombo amesema katika kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya viwanda kupitia kitengo cha utafiti na ushauri imefanikiwa kuendesha mafunzo mbalimbali ikiwemo ujasiriamali katika Kampas zote kwa wananchi,mafunzo ya wastaafu baada ya muda wao wa utumishi, ushauri wa kubuni vyanzo vya fedha endelevua pamoja na mafunzo kwa maafisa ununuzi wa Taasisi za Umma yanayolenga kufikia thamani ya pesa katika manunuzi yaa Umma.Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa Carolyne Nombo akitoa maelezo kuhusiana na mahafali ya 18 ya Taasisi hiyo kwa Kampas ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika Kampas ya Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza katika mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampas ya Dar es Salaam na Mtwara yalifanyika Viwanja Kampasi Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango akiwa katika picha ya Pamoja na Mameneja wa TIA mahafali ya 18 ya Taasisi hiyo.
Baadhi ya wahadhiri katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na wasio wahadhiri kwenye mahafali ya 18 ya Taasisi hiyo.
Baadhi ya wahitimu wakifatilia hotuba katika mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampas ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika kampas ya Dar es Salaam.
Wahitimu wakitunukiwa stashahada aliyekaa hapo ni mlemavu wa viungo kwenye mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampas ya Dar es Salaam.
Wahitimu wa shahada ya usimamizi wa biashara wakihudhurishwa shahada zao katika mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampas ya Dar es Salaam na Mtwara.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2