Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba (katikati,) akizungumza na wafanyakazi wa Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika ofisi ya wakala hiyo kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Geophrey Mizengo Pinda na kushoto ni Mkurugenzi wa bodi ya RITA Prof. Hamis Dihenga akifuatiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson, Leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson (kushoto,)akiwakaribisha Mawaziri wa Wizara ya Sheria na Katiba wakati walipotembelea ofisi ya Wakala hiyo kuona namna kazi zinavyoendelea pamoja na kutoa maelekezo ya kiutendaji, Leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA,) Prof. Hamis Dihenga (katikati) akizungumza na Waziri na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria mara walipotembelea ofisi za Wakala hiyo, Leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Wakala hiyo, katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Geophrey Mizengo Pinda na kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Emmy Hudson, Leo jijini Dar es Salaam.
Ziara ikiendelea.
Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Naibu wa Wizara hiyo Geophrey Mizengo Pinda wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa RITA mara baada ya kuwasili ofisini hapo na kushuhudia namna kazi zinavyofanyika, Leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba (kulia,) akipokelewa na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa RITA, Emmy Hudson mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo, Leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi (RITA,) Prof. Hamis Dihenga (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba mara baada ya kuwasili ofisini hapo, Leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Geophrey Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Leo jijini Dar es Salaam.
*Waipongeza RITA kwa utendaji kazi, wahaidi ushirikiano
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAZIRI wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba ameitaka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA,) kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na majukumu yanayotekelezwa na Wakala hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kufikia Mikoa mingi zaidi katika zoezi la usajili wa vizazi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Wakala hiyo Waziri Mwigulu amesema kuwa kazi zinazofanywa na Wakala hiyo ni kubwa na zinategemeana na taasisi nyingine ikiwemo Mamlaka ya vitambulisho vya utaifa na Uhamiaji hivyo ni vyema taarifa zote za usajili wa kila mwananchi zikasoma sawa katika ofisi zote zinazosajili na kuisaidia Serikali kupunguza gharama za kusajili wananchi pindi taarifa zao zinapohitajika.
"RITA ni kiungo muhimu sana na taarifa zote zinaanzia hapa hivyo mifumo ya taarifa lazima iongezewe nguvu kwa kuzirasimisha rasmi katika mfumo wa Serikali....mtu mwenye kitambulisho cha utaifa akienda katika Ofisi nyingine asianze kusajiliwa upya taarifa zake azikute kule, shirikianeni na taasisi nyingine kwa kushirikiana na watu wa tehama kujenga suala hili." Amesema.
Kuhusiana na utolewaji wa vyeti vya kuzaliwa Mwigulu ameipongeza Wakala hiyo kwa kuendelea kuifikia Mikoa mingi zaidi na amewaonya watendaji na raia wanaoshiriki kughushi vyeti hivyo kuacha mara moja.
"Kumpenyeza mtu asiye raia kupata cheti cha kuzaliwa ni kuihujumu Serikali, na Mtendaji yeyote na raia asiye mtendaji akishiriki hujuma hiyo atapata kile kinachofanana na uhujumu uchumi kwa mujibu wa Sheria." Amesema.
Aidha katika suala la mirathi amesema kuwa, Wakala hiyo ina jambo kubwa la kufanya katika suala hilo hasa kwa kuhakikisha mapungufu ya sehemu za sheria yanatatuliwa haraka na kurekebishwa na taratibu za kimila na imani zitengenezewe mazingira ya kisheria ili kuwafuata machozi wajane na yatima.
Vilevile amewataka kutunza kumbukumbu kwa Uzalendo wa hali ya juu na kwa kuzingatia sheria na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha pamoja na kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na viongozi wao.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geophrey Mizengo Pinda ameitaka Wakala hiyo kuendelea kutoa elimu zaidi kuhusiana na suala zima la mirathi ili kuweza kupunguza migogoro katika jamii.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment