Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amezitaka Taasisi za Fedha nchini kuhakikisha zinasaidia na kuwasukuma Wafanyabiashara wadogo kwa kuwapa mitaji ili kufikia malengo ya Uwekezaji nchini.
Prof. Kitila ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Taasisi mbalimbali za Fedha za TIB, Shirika la Maendeleo nchini (NDC) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).
Prof. Kitila amezitaka Taasisi hizo kuhamasisha Wafanyabiashara hao ambao wanaojihusisha na uuzaji na uchuuzi ambao hawazalishi mazao.
Pia Prof. Kitila amezitaka Taasisi hizo kuwasukuma Wafanyabiashara wadogo ili wafanye biashara hizo na baadae zitambulike ili kufikia malengo ya biashara za Viwanda vidogo vya utengenezaji na uzalishaji ili na wao wazalishe Ajira kwa wengine.
Kwa upande wake Mkrugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Charles Singili amehakikisha suala la kujitangaza zaidi kwa Wawekezaji baada ya Serikali na Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji Prof, Kitila kuhimiza suala hilo la kujitangaza kwa Taasisi hiyo ili kuvutia zaidi Uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine wamehakikisha kwa Waziri Prof Kitila na Serikali kutoa mitaji kwa Wafanyabiashara na kuwasaidia Watanzania katika Bishara zao ili kukuza Uwekezaji.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment