…………………………………………………………………
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,amekemea baadhi ya wawekezaji waache uhasama na kuwekeana chuki za kibiashara na badala yake washirikiane na kupendana ili kuinua sekta ya uwekezaji na viwanda mkoani hapo.
Akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa uwekezaji wa SAIBABA na kampuni ya Kichina ya Wen Xing kuhusiana na mgogoro baina ya wawekezaji hao ,Kibaha Mjini ,alimtaka mwekezaji SAIBABA kuacha vikwazo vitakavyo msababisha mwekezaji mwenzie ashindwe kuendeleza adhma ya serikali ya ujenzi wa viwanda.
Alisema ,tatizo kubwa alilofikishiwa ni mpaka,hoja ya madai ya SAIBABA kutaka malipo ya dola 25,000 sawa na sh.milioni 60 kwa kampuni ya Wen Xing .
“Sasa mkoa wa Pwani una jumla ya viwanda 1,200 na Wen Xing ni moja ya mwekezaji anaeongeza kiwanda ,sasa SAIBABA mkianza kelele zisizo za msingi ,wakati wenzenu wamechukua eneo ndani ya miezi saba na kujenga nyie mna miaka sita hamjajenga toka mchukue eneo 2015 mnanishangaza !!
” Acheni visa ,ugomvi wa kibiashara, mimi kama mkuu wa mkoa siwezi kukubali visa hivi ,alisema Ndikilo.
Ndikilo alielezea ,SAIBABA kwanza walikuja na hoja ya kampuni jirani hiyo kushindwa kununua eneo lao ,hoja ya pili kutiririsha maji na sasa hoja mpya kutaka malipo ya dola 25,000 kinyume na taratibu hatua iliyofikia kushtaki halmashauri hadi TAKUKURU .
Awali meneja wa Wen Xing, Yoyo alibainisha ujenzi ulianza July mwaka huu, umefikia asilimia 60 huku,madhumuni ya kiwanda ni kutengeneza viatu,na bidhaa za plastik ,”:;,ambapo ajira ya kwanza watu 100 na wanatarajia kufikiwa 500 baadae.
Nae meneja mradi SAIBABA ,Kanyilal Laxman alisema ,walinunua eneo mwaka 2015 na wanatarajia kuomba kibali cha kujenga Januari 2021.
Ofisa tarafa Kibaha Mjini,Anatoly Mhango aliwataka, wawekezaji wenye maeneo ambayo pori na mengine kutokujengwa kwa kipindi kirefu wavijenge kabla serikali haijachukua hatua ya kuvipokonya.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment