Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Tabu Shaibu(wa pilia kushoto) , Ofisa Msingi Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya wanachama wa Rotary Club wakiwa wameshika tuzo maalum ambayo imetolewa na manispaa hiyo kwa Club hiyo baada ya kukabidhi madawati 400 kwa shule mbili za msingi zilizopo katika Kata ya Chanika.
Ofisa Msingi katika Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas (wa kwanza kulia) Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Tabu Shaibu(katikati) pamoja na Mkurugenzi Miradi Kumail Manji kutoka Rotary Club wakimsikiliza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chanika Ladslaus Mutanda.
Gavana aliyemaliza muda wake Rotary Club Sharmila Bhatt akifafanua jambo.
Mshereheshaji Hamnza Kasongo ambaye pia ni mwanachama wa club hiyo akizungumza mbele ya viongozi wa manispaa ya Ilala, walimu, wanachama wa Rotary Club na wanafunzi wakati wa tukio la kukabidhi madawati.
Baadhi ya walimu kutoka Shule ya Msingi Chanika na Shule ya Msingi Tungini wakiwa kwenye tukio hilo.
Mkurugenzi Miradi Kumail Manji kutoka Rotary Club jijini Dar es Salaam akizungumza jambo kabla ya kukabidhi madawati kwa shule mbili za msingi zilizopo katika Kata ya Chanika.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi Chanika na Tungini wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa msaada na Rotary Club jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Chanika Ladslaus Mutanda(wa kwanza kushoto) akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi Miradi Kumail Manji (wa pili kushoto) .Wanaoshuhudia ni wanachama wa Club hiyo akiwemo Gavana aliyemaliza muda wake Rotary Club Sharmila Bhatt(wa tatu kushoto)
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Pepsi Paulo Richards akitoa salamu za kampuni yao kuhusu namna ambavyo wanaamini msaada huo wa madawati unavyokwenda kuboresha mazingira mazuri ya wanafunzi kupata elimu.
Mkurugenzi Miradi Kumail Manji (wa kwanza kulia) akiwa na wanachama wengine wa Club hiyo wakisiliza maelezo wakati wa tukio hilo la kukabidhiwa kwa madawati 400 kwa shule mbili za Kata ya Chanika.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Tabu Shaibu(kulia) na Ofisa Msingi katika Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas(kushoto) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mradi wa Rotary Club Kumail Manji(hayupo pichani) kuhusu uamuzi wao wa kusaidia madawati hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Tabu Shaibu akizungumza mbele ya wanafunzi, walimu na wanachama wa Rotary Club ya Dar es Salaam wakati wa tukio la ukabidhiwaji madawati 400 kwa shule mbili za msingi zilizopo kata ya Chanika Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Tabu Shaibu akizungumza mbele ya wanafunzi, walimu na wanachama wa Rotary Club ya Dar es Salaam wakati wa tukio la ukabidhiwaji madawati 400 kwa shule mbili za msingi zilizopo kata ya Chanika ===== ====== ====== ======
Na Said Mwishehe, Michuzi Blog
ROTARY Club jijini Dar es Salaam imekabidhi madawati 400 kwa shule mbili za msingi zilizopo katika Kata ya Chanika ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule mbalimbali jijini.
Madawati hayo yamekabidhiwa katika Shule ya Msingi Chanika na Shule ya Msingi Tungini ikiwa ni sehemu ya klabu hiyo kutekeleza ahadi yao ya kuondoa changamoto ya madawati kwa shule za misngi.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa kwa madawati hayo, Kaimu Mkurugenzi katika Halmashaur ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Tabu Shaibu amewashukuru wanachama wa Klabu ya Rotary kwa msaada huo wa madawati 400 ambayo kwa sehemu kubwa yamekwenda kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika shule hizo.
Amesema klabu hiyo imeonesha kwa vitendo namna ambavyo imeamua kusaidia jamii na kwamba madawati hayo yanakwenda kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kupata elimu lakini pia na walimu kuwa na mazingira mazuri ya kutoa elimu waliyonayo na kuipandikiza kwa watoto hao kwa faida yao na Taifa kwa ujumla hasa kwa kuzingatia elimu ndio msingi wa maisha.
Aidha amesisitiza madawati hayo yatatunzwe ili yaweze kuwasaidia na wengine huku akitumia nafasi hiyo kwa sehemu kubwa kuwashukuru Rotary kwa kutoa madawati hayo.Pia amewashauri iwapo wataweza kusaidia katika maeneo mengine yakiwemo ya afya, na mazingira.
Awali Ofisa Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Elizabeth Thomas amesema katika halmashauri hiyo kumekuwepo na ongezeko kubwa la sana la wanafunzi hasa katika maeneo haya ambayo ni mji mpya, mpaka sasa halmashauri yao ina wanafunzi 197,000 na kila mwaka kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanajiunga na elimu ya msingi.
Amesema mwaka 2019 waliandikisha wanafunzi 28,000 na mwaka 2020 wameandikisha wanafunzi 32,000 kuingia darasa la kwanza, hivyo maana yake kunakuwa na ongezeko la wanafunzi pamoja na kwamba kuna na changamoto ya awali ambayo unasema nimepata kutatua , linapongia kundi jingine la wanafunzi inaongezeka badala ya kupungua.
"Lakini ninyi kama wadau wetu mmekuwa mstari wa mbele kutusaidia, tumeona mmechimba visima vingi vya maji sehemu mbalimbali , hapa Chanika mmetengeneza darasa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum , leo hii mmevuja rekodi kubwa kwa kutupatia madawati mengi katika shule zetu mbil i.
"Katika bajeti yake Mkurugenzi mwaka huu alipanga kutengeneza madawati 3,000 tu kwasababu anahitajika pia kujenga madarasa ya msingi na sekondari, madawati ya msingi na sekondari , leo hii ninyi kama familia yetu mmeweza kutuletea madawati 400, kwa kweli ni ongezeko kubwa ambalo sisi hatukulitarajia.
"Wanafunzi wetu kwa madawati 400 ambapo kila dawawati watakaa watatu maana yake wanafunzi 1,200 watakaa kwenye madawati wakiwa wametulia, tunawashukuru kwasababu mmetuboreshea mazingira ya kujifunzia , watoto na sasa watajifunza kwa hara,"amesema Thomas.
Pia amewahimiza walimu wa Chanika wa shule hizo mbili kuhakikisha madawati hayo analindwa , ili kuwapa heshima waliowapatia."Madawati haya yana namba hivyo watoto watakaoka kwenye madawati ndio watakuwa walinzi, tukikuta dawati limeharibika wanafunzi wanaolikaa ndio watakaohusika kutengeneza maana kuna wanafunzi watundu, wanafungua skuruu na kisha kwenda kuuza".
Akizungumzia kuhusu maada huo wa madawati Gavana wa Klabu ya Rotary jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Miradi Kumail Manji amesema wamesaidi madawati hayo baada ya kupata ombi la kutoka katika shule hizo ambazo zilikuwa zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati.
"Hivyo tukasema lazima tusaidie na tumeanzia hapa , tuliambiwa huko nyuma kuna uhaba wa madawati zaidi ya 15000 katika Jiji la Dar es Salaam , na kwa maana hiyo kuna haja kubwa kukidhi mahitaji, hivyo sisi tukachukua dhamana na tukaanzisha hu mradi ambapo tumedhamiria kusambaza madawati karibia 1000.
"Madawati 1000 maana yake ni nini? Dawati moja wanakaa wanafunzi watatu, hivyo tutakuwa tumewezesha wanafunzi 3,000 kukakaa kwenye dawati.Shule hizi mbili za Chanika,"amesema.
Wakati huo huo Mwakilishi kutoka Kampuni ya Pepsi Paulo Richards amesema kukabidhiwa kwa madawati hayo kwa shule hizo ni matumaini yao wanafuzi wanakwenda kuwa katika mazingira mazuri ya kupata elimu."Pepsi tunaamini baada ya kutolewa kwa madawati haya wanafunzi wanakwenda kusoma vizuri na kutakuwa na matokeo mazuri hapo baada.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Chanika Ladslaus Mutanda ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa kupata madawati hayo ambayo yaakwenda kumaliza changamoto ya uhaba wa madawati katika shule yao.
"Kwa idadi ya vyumba tulivyonavyo humo ndani watoto watakaa chini kwasababu ya wingi wao lakini sio kwa kukosa dawati, vyumba vyote sasa vitajaa madawati , kwa hali hiyo hatutarajii watoto wakae chini,"amesema na kutoa ombi kwa klabu hiyo kama wataweza kuwasaidia kuwajengea uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao wapo shuleni hapo wapatao 67.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment