TAASISI zinazo simamia Sekta ya usafiri nchini zimetakiwa kuendelea kutumia ubunifu wa kiteknolojia katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga ili kuweza kufikia viwango vya kimataifa na baadae kuwa na soko la uhakika.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) Silvester Mpanduji wakati akifungua Kongamano la saba la wanataaluma wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa mwaka 2020, lililoambatana na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wanaohimu waliofanya vizuri katika masomo yao.
Amesema, pamoja na mafanikio ambayo yamepatikana kwenye sekta hiyo lakini ipo haja ya kuiongezea nguvu ya Teknolojia ili iweze kufika mbali zaidi hasa katika soko la dunia.
Aidha Mpanduji amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini hususani vya ufundi kuacha kutegemea kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo yao badala yake watumie maarifa waliyoyapata kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia kuendesha maisha yao.
Amesema katika kipindi chote cha masomo wanafunzi wamejifunza vema hivyo wanapomaliza wanapaswa kwenda kuutumia ujuzi huo kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na Sido itakuwa tayari kuwasaidia kwa kuwawezesha kuwapa mafunzo zaidi, mikopo na kuwaunganisha na taasisi mbalimbali.
Naye Mkuu wa chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa amesema chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo ambazo pamoja na kuwapatia ajira vijana lakini kimekua ni chachu ya wahitimu kuweza kutengeneza fursa za kujiajiri katika maisha yao ya kila siku.
Ameongeza kuwa, mafunzo ya ndege yanayotolewa chuoni hapo yanasimamiwa na Shirika moja la Kimataifa na hivyo kiwango cha wahitimu wanatoka hapo ni cha Kimataifa.
."Niwahahakishie wahitinu hawa wanauwezo wa kushindana na wale waliosoma nchi zingine na tunaamini kuingia kwao kwenye soko kutabadirisha kabisa tasnia ya anga iweze kuongeza mchango wake mkubwa kwenye uchumi wa nchi hasa kwenye sekta ya utalii na zile za madini na mafuta na gesi ambapo watu hao wanatakiwa kusafiri kwa haraka sana," alisema.
Aidha alisema gharama kubwa ya kusomea uhandisi wa ndege imekuwa ni changamoto ambayo hupelekea kuzalisha wataalamu wa usafiri wa anga wachache.
Nae Mohamed athumani mhitimu wa diploma ya Mechanical engineering amesema, elimu aliyoipata chuoni hapo itamuwezeaha kuingia kwenye soko la ajira kwa kujiajiri ama kuajiliwa na kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake, Joseph Mwaijage muhitimu wa bachelor Automobile engineering amesema mafunzo wanayoyapata pale yamekuwa yakiwajengea uwezo vijana wengi kujiajiri hata kuanzisha miradi mbali mbali bila ya kufanya makosa.
"Tunawashauri wenzetu ambao wanafanya kazi za kihandisi mitaani, mfano gereji, kufika chuoni hapa na kupatiwa ujuzi zaidi na kujifunza kwenye njia rasmi".
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment