TCCIA KUWAFIKIA WAFANYABIASHARA 3000 KUTATUA CHANGAMOTO ZAO | Tarimo Blog

Meneja wa mradi unaojulikana kwa jina la kujenga daraja Kati ya sekta binafsi na sekta ya umma  Beatrice Minde akiwa anawapa mafunzo baadhi ya wafanya biashara waliofika katika semina iliyowashirikisha wafanyabiashara wa jiji la Arusha ili kutambua changamoto wanazozipitia semina ulioandaliwa na Chama Cha wafanyabiashara wa viwanda mkoa wa Arusha TCCIA kwa kushirikiana na shirika la Trias semina uliofanyika Ndani ya jiji la Arusha juzi. (Picha na Woinde Shizza, ARUSHA)

Na Woinde Shizza, Michuzi TV -ARUSHA
CHAMA Cha wafanyabiashara wa viwanda mkoa wa Arusha TCCIA kwa kushirikiana na shirika la Trias kwa pamoja wamelenga kuwafikia wafanyabiashara wapatao 3000 kutambua changamoto wanazozipitia ili kuweza kushirikiana na serikali kuboresha ufanyaji wa biashara nchini.

Akizungumza katika semina iliyowashirikisha wafanyabiashara wa jiji la Arusha Meneja wa mradi unaojulikana kwa jina la kujenga daraja Kati ya sekta binafsi na sekta ya umma Beatrice Minde amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya ufadhili kutoka umoja wa Ulaya.

Alisema kuwa msingi mkubwa wa maoni hayo utasaidia serikali kupitia Wizara ya Fedha katika utungaji na uboreshaji wa sera na kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara nchini

Alisema mradi huo Ni wa miaka miwili umeanza mwezi January mwaka huu katika mikoa 10 lengo likiwa Ni kutambua changamoto za wafanyabiashara na baadae kuwasilisha serikalini kwa lengo la kutatuliwa na kufanyiwakazi na kuleta Tija katika kunyanyua sekta ya biashara nchini 

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Nebart Mwapwere amesema wao Kama daraja la kuwaunganisha wafanya biashara wameamua kufanya utafiti huo kwa kuwafikia wafanyabiashara kwa njia ya tehama au kieletroniki ambayo hukusanya maoni juu ya changamoto zinazowakabili. 

Alisema kuwa wamefikia mikoa 10 ikiwa ni Sera ya serikali ya awamu ya tano inayolenga kuboresha kutatua changamoto za wafanyabiashara wa kila Aina wakiwemo na wamiliki wa viwanda kutambua namna ya kufikisha mawazo yao kwa viongozi husika na kufanyiakazi ndio lengo la kufanya mijadala na wafanya biashara hapa nchini.

Alisema Kama wafanyabiashara wengi wa viwanda wamelalamikia kutozwa Kodi kubwa na kuwepo na utitiri wa malipo ya Kodi na kusema kuwa umeme nao ni sehemu ya matumizi makubwa ya uendeshaji wa viwanda na kutaka kupata punguzo kutoka serikalini.

Nae Slyvester Kazi Meneja Mauzo na Masoko ya Nje kutoka kampuni ya A to Z alisema kuwa Rais Dkt.John Magufuli anataka kuzalisha mabilionea wapya na semina hiyo ni mkakati wa serikali kuwakomboa wafanyabiashara wa kati na wa chini kufikia malengo ya kuwa mabilionea wapya.

Alisema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuwashirikisha kutoa changamoto zao na nini kifanyike hii inaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kufikia malengo na maono ya Rais wetu ikiwa ni utekelezaji wa sera ya uchumi wa kati wa viwanda.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2