Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KUNDI la Vijana wa kada mbalimbali limeaswa kuzidisha mapambano dhidi ya Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (HIV/AIDS) kutokana na wao kuwa Wahanga wakubwa wa Maambukizi hayo yanayoshambulia zaidi kundi hilo.
Akizungumza wakati wa Hitimisho la Kongamano la Vijana hao lililoangazia masuala ya Kiafya, Kiroho na Kiuchumi lililofanyika jijini Dar, Diwani wa Kata ya Zingiziwa, Maige Maganga amekiri kuwa Virusi vya Ukimwi bado ni tishio kwa jamii haswa Vijana, amewaasa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi hayo na kuchunga Afya zao kwa umakini.
“Tahadhari si katika mahusiano peke yake, bali hata kwenye vifaa tunapoenda kupata huduma zetu,akina Dada kwenye kutengeneza Kucha zenu, matumizi ya vitu vyenye ncha kali, sisi wote lazima tuwe na tahadhiri kubwa na makini,” amesema Diwani Maganga.
Meneja wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Victoria Huburya amesema kila mtu anawajibu kuzidisha mapambano dhidi ya Maambukizi hayo bila kujali umri, nafasi na Jinsia katika jamii inayomzunguka.
Huburya amesema NACOPHA ina kazi ya kuhakikisha Jamii inaondokana na Unyanyapaa, kuhamasisha Upimaji wa HIV na Matumizi sahihi ya Dawa za kufubaza maambukizi hayo (ARV), amesema suala hilo la mapambano dhidi ya maambukizi hayo linaibeba jamii katika masuala ya utoaji wa Huduma za Afya ikiwa sambamba na kuhusisha Serikali, Dini, Jamii na Mifumo ya Kijinsia.
“Dhana potofu zinachochea tatizo hili, zinajengwa na Mila na Tamaduni tulizonazo, wapo wanaodhani kuwa kupata Maambukizi hayo kuwa na Wapenzi wengi, hapana! pengine huyu mtu amezaliwa na maambukizi hayo au mtu wake wa kwanza (Mke) wa Ndoa ya halali kabisa ndiye aliyemuambukiza au kupata ajali”, amesema Huburya.
“Unyanyapaa katika jamii unavuruga utaratibu wa shughuli za muitikio wa Ukimwi kwa sababu inapelekea Watu kuogopa kupima Afya zao, kutumia Dawa, na kushindwa kujitokeza kusema hali zao”, ameeleza Huburya.
Naye Mwenyekiti wa NACOPHA, Konga ya Ilala, Mchungaji Emanuel Msinga amesema ameanza juhudi hizo za utoaji hamasa kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutokana na kuona kundi kubwa la Vijana kuwa Wahanga wakubwa na kupelekea kuathiriwa zaidi Kiuchumi, Kiakili katika Taifa na kupoteza nguvu kazi.
“Kwa upande wangu kama Kiongozi wa Dini nimefurahishwa na mwenendo wa Viongozi wenzangu kuahidi kuhamasisha mapambano haya dhidi ya Virusi vya Ukimwi katika Jamii kupitia mafunzo ya Viongozi wa Dini mbalimbali, kule Arusha”, amesema Mchungaji Msinga.
Kwa upande wake, Mhamasishaji, Victor R. Kalinga amesema Vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 19 na miaka 19-35 hadi miaka 45 ndio wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi hayo.
“Mimi nipo katika mfumo wa kuchukua Dawa za kupunguza makali ya VVU kwa kipindi cha baada ya miezi mitatu kwa sasa miezi Sita, huwa naenda kuchukua Dawa hizo na kuwatafuta zaidi vijana, naona hakuna vijana katika mfumo wa Uchukuaji Dawa (CTC), vijana hawa wanagopa wanaamini Ukimwi ni mkubwa kuliko wao hivyo wameamua kuishi hivyo,” amesema Victor.
Victor amewaasa kujitokeza kwa wingi katika kutambua Afya zao na kuchukua maamuzi sahihi pale wanapokutwa na maambukizi hayo au kuchukua tahadhari pale unapogundua kuwa Hassan Maambukizi.
Mafunzo hayo yalianza mwezi May mwaka huu kwa vijana 20 kupatiwa mafunzo baadae hadi kufikia Vijana 266 kupata Elimu ya Kiafya, Kiuchumi na Kiroho katika Jamii inayowazunguka na baadae kutunukiwa Vyeti, kupitia Mradi wa HEBU TUYAJENGE unaotekelezwa na Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) chini ya Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekeni (USAID).
Baadhi ya Vijana walioshiriki Kongamano hilo lililoangazia masuala ya Kiafya, Kiroho na Kiuchumi llilofanyika jijini Dar Es Salaam.
Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Zingiziwa, Maige Maganga (aliyevaa Koti la Rangi ya Kijivu) akikabidhi Cheri kwa mmoja wa Washiriki wa Mafunzo maalum ya Vijana yaliyoangazia masuala ya Kiafya, Kiroho na Kiuchumi yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Victoria Huburya akizungumza katika Jopo la pamoja lililohusisha Viongozi wa Dini, Washauri na Wakufunzi wa Ujasiriamali katika Kongamano la Vijana lililoangazia masuala ya Kiafya, Kiroho na Kiuchumi llilofanyika jijini Dar Es Salaam.
IMG 5877: Mwenyekiti wa NACOPHA, Konga ya Ilala, Mchungaji Emanuel Msinga akichangia jambo wakati wa Jopo la pamoja wakati wa Kongamano la Vijana lililoangazia masuala ya Kiafya, Kiroho na Kiuchumi llilofanyika jijini Dar Es Salaam.
Mhamasishaji, Victor R. Kalinga akichangia maada katika Kongamano la Vijana lililoangazia masuala ya Kiafya, Kiroho na Kiuchumi llilofanyika jijini Dar Es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment