WACHUNAJI NGOZI WAPEWA MAFUNZO NA KUPATIWA LESENI | Tarimo Blog

 
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe kutoka Idara Uzalishaji na Masko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Gabriel Bura akizungumza kuhusiana na uandaji wa mafunzo kwa wachunaji Ngozi wa Machinjio ya Vingunguti ,jijini Dar es Salaam.
Mwakilillshi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam ambaye Afisa Biashara wa Mkoa huo Thabit Massa akifunga mafunzo  na utoaji wa leseni ya wachunaji Ngozi wa Machinjio ya Vingunguti , jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja  na wataalam na wachunaji Ngozi wa Machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Mwakilillshi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Afisa Biashara Mkuu wa Mkoa Thabit Massa akimkabidhi leseni ya uchunaji Ngozi Manyika Mazenga Mara baada ya kufunga mafunzo kwa wachunaji Ngozi Machinjio ya Vingunguti ,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wachunaji Ngozi wa Machinjio ya Vingunguti wakipata mafunzo ya uchunaji yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

UONGOZI  wa Mkoa wa Dar es Salaam umesema kuwa wachunaji Ngozi wa Machinjio ya Vingunguti watumie nafasi hiyo vizuri kutokana na kujengwa Kiwanda katika Machinjio hayo.

Hayo ameyasema Mwakilishi Katibu Tawala wa Mkoani wa Dar es Salaam ambaye Afisa Biashara Mkuu wa Mkoa huo Thabit Massa wakati wa Utoaji wa leseni kwa wachunaji Ngozi wa Machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa uchunaji Ngozi ni fani hivyo wanatakiwa kutumia mafunzo hayo kwa weledi kwa kuhakikisha Ngozi inapata ubora na kuweza kuingia katika masoko ya kikanda bila vikwazo.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya mifugo imegharamikia katika kutoa mafunzo ili kuweza kupata Ngozi zenye ubora na hatimaye kuweza kupata mapato yake halisi pamoja na kuwa na soko la viatu.

Massa amesema hakuna sababu ya mtu kuharibu Ngozi kwani faini yake ni kubwa ikiwa ni kutaka watu kutumia weledi katika kufanya uchunaji wa Ngozi kuwa bora na kuondoa vikwazo vinavyotokana na bidhaa ya Ngozi ya kuwa haina ubora kutokana na uchunaji wa mbovu.

Amesema Mkoa itaendelea kushirikiana na wachunaji Ngozi Pamoja na kutaka kuwa na umoja uimara wa wenye katiba kuweza kukopesheka kwa kutumia makundi.

Thabit amesema ujenzi wa Kiwanda cha machinjio kutakuwa na viwanda vingine vidogo vidogo ikiwemo Kiwanda cha kutengeneza vifungo kwa kutumia kwato za mifugo ya Mbuzi, Kondoo pamoja na Ng'ombe.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo,Usalama wa Chakula na Lishe katika Idara ya Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Gabriel Bura amesema kuwa faini ya kutoboa Ngozi ni sh.milioni moja hivyo wachunaji wanatakiwa kuwa na uangalifu.

Amesema bidhaa ya Ngozi ina fedha nyingi lakini inapotea kutokana na uchunaji usiozingatia weledi kutokana na watu kukosa mafunzo ndio serikali imejizatiti kuandaa mafunzo na kutoa leseni.

Bura amesema kuwa mafunzo hayo ni endelevu kwa kuwafikia wachunaji wote.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2