WATAALAMU WA MAJI MUACHE KUFANYA KAZI KWA MAZOEA, DAWASA KUPELEKA MAJI GOLANI | Tarimo Blog

 

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka wataalamu wote kutoka Mamlaka za Maji nchini kuacha kuzoea shida za wananchi.

Hayo ameyasema leo alipotembelea Kata ya Golani Mtaa wa Mnazi mmoja Wilaya ya Ubungo akiwa ameambatana  na Mbunge wa Jimbo hilo Prof Kitila Mkumbo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Akiwa katika Mkutano na wananchi wa kata hiyo, Aweso amesema kuwa Watalaamu hawatakiwi kuzoea shida za wananchi kwani jukumu lao ni kuhakikisha wanawatumikia kwa jitihada zote.

Aweso amesema,  Dawasa kwa mkoa wa Dar es Salaam wamefanya kazi kubwa ila ukiangalia katika ripoti zao za mjini ni nzuri changamoto kubwa ipo pembezoni mwa mji. Amesema, "nimeambatana na Mtendaji Mkuu wa Dawasa atuambie leo hapa maji yanakuja Golani na kama yanakuja ni lini?" 

Aidha, Aweso amesema jana niliwaagiza Dawasa wafanye mabadiliko ya mameneja na hapa kwenu Ubungo tayari wameshafanya naamini atakuja kufanya kazi kwa weledi.


Kwa upande wa  Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema katika eneo la Ubungo kulikua na changamoto maeneo ya Kwembe, Kifuru na Golani na hiyo ni kutokana na Dawasa kutumia pesa za ndani katika kujenga miradi.

Amesema, changamoto ya Golani ni Milima na kunahitaji  bomba la peke yake na kazi hiyo tutaianza baada ya sikukuu na tayari wameshafanya usanifu wa mradi wa Km 3.7 

"Kazi imeshaanza, na baada ya muda mfupi maji yatakuwa yameshafika wananchi kuanza kupata huduma ya maji safi na salama," amesema Luhemeja.

Akiongelea upatikanaji wa maji pembezoni mwa mji, Luhemeja amesema tayari miradi mbalimbali  inaendelea kwani tayari wamepata mkopo kutoka benki ya dunia kwa miradi ya maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akichimba shimo kwa ajili ya kutandika mabimba ya DAWASA wakati wa uzinduzi wa zoezi la uchimbaji kwa ajili ya kutandika mabimba ya DAWASA yatakayoweza kumaliza tatizo la maji katika katika eneo la Mnazi Mmoja kata ya Golani Wilayani Ubungo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) na Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila A.K.Mkumbo   akichimba shimo kwa ajili ya kutandika mabimba ya DAWASA yatakayoweza kumaliza tatizo la maji katika katika eneo la Mnazi Mmoja kata ya Golani Wilayani Ubungo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akiondoa udongo wakati wa uzinduzi wa uchimbaji na utandikaji wa mambomba utakaoweza kumaliza changamoto ya maji iliyokuwa inawakabiri wakazi wa eneo la Mnazi Mmoja kata ya Golani Wilayani Ubungo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa kuhusu namna Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli wanawapatia maji katika maeneo mbalimbali likiwemo eneo hilo la Kata ya Golani Mtaa wa Mnazi mmoja Wilaya ya Ubungo wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya Maji katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) na Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila A.K.Mkumbo akizungumza na wananchi kuhusu namna alivyojipanga kumaliza shida ya maji katika Kata ya Golani hasa katika mtaa wa Mnazi Mmoja wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso ya kukagua miundombinu ya Maji katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akijibu hoja za waziri wa Maji pamoja naza wananchi kuhusu namna shirika hilo lilivyojipanga na kuhakikisha upatikanaji wa maji katika Kata ya Golani hasa katika mtaa wa Mnazi Mmoja wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso ya kukagua miundombinu ya Maji katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Wananchi wa Mtaa wa Mnazi Mmoja katika Kata ya Golani wakiuliza maswali kwa DAWASA kuhusu upatikanaji wa maji katika eneo hilo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso ya kukagua miundombinu ya Maji katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano uliokuwa na lengo la kuwaondolea hadha ya upatikanaji wa Maji katika eneo la Mnazi Mmoja kata ya Golani Wilayani Ubungo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso ya kukagua miundombinu ya Maji katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitolea ufafanuzi kuhusu namna uchimbaji na utandikaji wa mabomba katika eneo la Mnazi Mmoja kata ya Golani Wilayani Ubungo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso ya kukagua miundombinu ya Maji katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akichimba Shimo kwa ajili ya kutandaza mambomba ya Maji ya DAWASA katika eneo la maungio lililopo katika eneo la Kimara Mwisho litakalopeleka maji katika eneo la Mnazi Mmoja kata ya Golani Wilayani Ubungo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha bomba la kuungia Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) na Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila A.K.Mkumbo lililopo katika eneo la KImara Mwisho.
Muonekano wa Bomba litakalounganisha bomba la kwenda eneo la Mnazi Mmoja kata ya Golani Wilayani Ubungo.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2