Bweni lililochomwa moto 2018 laungua tena, kura zapigwa kubaini mhusika | Tarimo Blog

Na Amiri Kilagalila, Njombe
SEHEMU ya bweni la wavulana wa shule ya sekondari Mang'oto wilayani Makete Mkoani Njombe, imeungua moto na kusababisha hasara ya baadhi ya vifaa vilivyokuwemo katika bweni hilo.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronika kessy ametembelea katika shule hiyo na kusikitishwa na tukio hilo ikizingatiwa kuwa bweni hilo liliwahi kuungua kwa kuchomwa moto na mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo mwaka 2018 na ameagiza kuchukuliwa hatua mara moja.

“Nilipopokea taarifa za kuungua kwa bweni la Mang’oto, nimepatwa na mfadhaiko kwasababu bweni hili liliungua mwaka 2018 mwezi wa 3 na tukafanya jitihada kubwa kuchangisha wananchi, wadau ili kuweza kutoa fedha na kurudisha hili bweni sehemu yake, sasa katika kipindi cha miaka miwili bweni linaungua tena katika mazingira yale yale.”Alisema Veronika

Kamati ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na maafisa wengine wa serikali wamefika katika shule hiyo ambapo katika hatua za awali limendeshwa zoezi la kupiga kura ili kuwabaini wahusika na baada ya zoezi hilo kamati hiyo imeondoka na wanafunzi kadhaa kwa mahojiano zaidi.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronika Kessy amesema hatua hizo ni za awali huku akiwataka wanafunzi wanaowafahamu waliofanya kitendo hicho kutoa ushirikiano kupitia kwa walimu wao.
“Kama kuna mtu mnamfahamu amefanya hicho kitendo mumfuate mwalimu wa malezi, nenda ukamwambie itakuweka huru.”  Aliwaeleza wanafunzi

Afisa elimu mkoa wa Njombe mwalimu, Gift Kyando amewaeleza wanafunzi kutambua wajibu wao wawapo shuleni.

“Ukasirike vyovyote lakini sio kuchoma bweni wala kuchoma darasa, ninyi mmechoma bweni mara ya pili sasa, wazazi wenu huko wanahangaika wewe unachoma mahala pa kulala.” Aliwaeleza wanafunzi mwalimu Gift Kyando

Afisa elimu wa kata hiyo Furaha Kyando amemteua mwalimu Jacob Mdibwa kusimamia shule kwa kipindi ambacho uchunguzi unaendelea juu ya tukio hilo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2