WAZIRI MKUU ATOA AGIZO UENDELEZAJI ZAO LA MKONGE | Tarimo Blog

 





WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Jumatano, Januari 20, 2021 amekagua kitalu cha miche ya mkonge cha TARI Mlingano lililopo wilayani Muheza, Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche kwa wakulima wa zao hilo.

Akizungumza wakati wa tukio hilo Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche ya mkonge

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI Mlingano ili kukiwezesha kupanua eneo la uzalishaji miche kwa kununua vitendea kazi yakiwemo matrekta.

Amesema kituo cha TARI Mlingano kinatakiwa kijikite katika kufanya  utafiti wa mbegu bora pamoja na dawa za kudhibiti magonjwa katika zao hilo na suala la uzalishaji wa mbegu lifanywe kwa ushirikiano katika ya kituo hicho na wadau wa zao hilo.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Januari 20, 2021) baada ya kukagua
kitalu cha miche ya mkonge la TARI Mlingano lililopo wilayani Muheza,
Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche kwa wakulima wa zao hilo.

Waziri Mkuu amesema ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche
ya mkonge nchini kila halmashauri na wakulima wakubwa wanatakiwa
watenge ekari 10 kwa ajili ya kuandaa vitalu vya miche ya mkonge na
kugawa kwa wananchi kwenye maeneo yao.

Amesema kituo cha TARI Mlingano kinatakiwa kijikite katika kufanya
utafiti wa mbegu bora pamoja na dawa za kudhibiti magonjwa katika zao
hilo na suala la uzalishaji wa mbegu lifanywe kwa ushirikiano katika
ya kituo hicho na wadau wa zao hilo.

Kadhalika, alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mpaka ifikapo
mwakani kuwa na ongezeko la uzalishaji wa miche zaidi ya Milioni mbili
ya sasa kwani mahitaji ni makubwa kwa sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha
Mlingano, Dkt Catherine Senkoro amesema hadi kufikia Januari, 2021
jumla ya hekta 32.6 sawa na ekari 81.5 zimepandwa miche ya mkonge
katika maeneo ya TARI Mlingano.

Amesema kituo chao kwa kushirikiana na Bodi ya Mkonge Tanzania imetoa
mafunzo kwa wakulima na Maafisa Ugani katika baadhi ya mikoa inayofaa
kwa kilimo cha mkonge ambayo ni Tanga, Morogoro, Pwani, Kilimanjaro,
Lindi, Simiyu, Shinyanga na Mara. “Kufikia Desemba 2020, wakulima 422
na Maafisa Ugani 840 katika mikoa hiyo walipatiwa mafunzo.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 Wizara
ya Kilimo kupitia kituo cha TARI Mlingano imepanga kuzalisha miche
4,000,000 katika vitalu vyake, pia itapanua maabara ya uzalishaji wa
miche kwa njia ya chupa  ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa miche.
Utaratibu huo unakadiriwa kuchangia miche milioni 10 kwa mwaka.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2