DC NAMTUMBO AWATAKA ASKARI WA AKIBA KULINDA AMANI | Tarimo Blog



Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo  

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo  mkoani  Ruvuma  Sophia  Mfaume  Kizigo
amewataka  wahitimu  wa mafunzo ya askari wa akiba  katika kijiji
cha Limamu wilayani humo  kuilinda amani  ya nchi  yetu  kwa kutoa
taarifa dhidi ya wahalifu  au kuwakamata  wahalifu  wenye  nia mbaya
na amani ya nchi yetu.

Kizigo  amewataka  kuwa  askari  wema wenye kufuata sheria  za kazi
zao katika kuisaidia serikali  huku akiwataka pia wasijiingize  katika
 kupokea rushwa  katika kazi zao kwa kuwa rushwa  ni adui Wa haki
katika jamii.

“Tunawategemea  katika  kuwakamata  waweka  mimba  wanafunzi, hivyo
mkijihusisha  na upokeaji rushwa  mtasababisha kutowakamata wahalifu
na nafasi  ya kazi yako  haitakuwa na manufaa  kwa jamii  na hata kwa
serikali. “ alisema Kizigo.

Ofisa  mtendaji wa  kijiji  cha  Limamu  bi. Agnes  Nchimbi  alisema
kuwa  vijana  waliojiandikisha  katika kujifunza Mgambo  walikuwa  140
lakini kutokana na sababu zisizozuilika za kiafya  vijana wengine
waliacha  na kubakiwa na vijana 91 ndio waliohitimu mafunzo hayo
katika kijiji chake.

Pancras  Newa  mhitimu  wa mafunzo hayo  alisema  walianza mafunzo
mwezi  mei  2020 na kuhitimu  mwezi  januari  2021  hivyo  aliiomba
serikali kuendelea  kutoa mafunzo  kwa vijana  wengine  kwa kuwa
mafunzo hayo  yanawafanya vijana wawe  wakakamaVu  , kuzijua mbinu
mbalimbali za kivita pamoja  na kujua kutumia  silaha  alisema Newa.

Naye mwenyekiti wa  kijiji cha Limamu  bwana  Magnus  Ndunguru
alisema walihamasisha  vijana kujiunga na Mgambo  katika kijiji hicho
kupitia  mikutano ya  hadhara ya  kijiji   na kuwapata  vijana 140
lakini kulingana na matatizo ya kiafya  walibahatika kuhitimu ni hao
91.

Sherehe  ya kuhitimu  mafunzo ya  jeshi la akiba  katika kijiji cha
limamu  yalifanyika katika  uwanja  wa shule ya msingi  Tumaini
ambapo  mkuu wa wilaya ya Namtumbo  alipokea viapo vya askari  wa
akiba hao  pamoja na kukagua gwaride lililoandaliwa na askari hao wa
akiba.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2