MJUMITA WATOA MAFUNZO YA UTAWALA BORA NAMTUMBO | Tarimo Blog



Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo  

MPANGO  wa jamii  wa usimamizi  wa misitu  Tanzania (MJUMITA) unatoa
mafunzo  ya utawala bora  kwa  vijiji  viwili vinavyoshiriki  katika
usimamizi shirikishi  wa misitu  katika wilaya ya Namtumbo  mkoa  wa
Ruvuma  katika kijiji  cha Kilangalanga na Limamu.

Mafunzo hayo   ya siku nne  kuanzia tarehe 18 mwezi huu na yataishia
tarehe 22 mwezi huu, yakiwa na lengo la kuiwezesha kamati ya maliasili
ya kijiji kufahamu  majukumu yao ya kila siku,wafahamu  majukumu ya
serikali, wafahamu majukumu ya wadau  pamoja na kujua  kusimamia
,kutunza  hesabu  za  serikali kitaalamu.

Stanley  Baluweshi  mwezeshaji  wa mafunzo kutoka ngazi ya
Halmashauri ya wilaya ya  Namtumbo alisema katika vijiji hivyo  viwili
wajumbe 10 kutoka kila kijiji wanaohusika  na kamati  ya  usimamizi
wa  maliaasili katika kijiji ndio walengwa  wa mafunzo hayo.

Agnes  Nchimbi mtendaji wa kijiji  cha Limamu ambaye ni  mshiriki wa
mafunzo hayo  amedai kijiji chake kipo katika mpango  wa jamii wa
usimamizi wa misitu  hivyo mafunzo hayo  yatawawezesha  kuzifahamu na
kuzifuata taratibu zilizowekwa  na  serikali  ili kuepuka migogoro
isiyo ya lazima  katika jamii.

Nchimbi aliwataja wajumbe  waliohudhuria katika mafunzo hayo  kutoka
katika kijiji chake  kuwa ni Yeye  ambaye ni mtendaji wa kijiji,
mwenyekiti kamati  ya maliasili,katibu wa kamati,mweka hazina ,kamanda
kamati ya maliasili  pamoja na wajumbe  wa 5 kutoka  katika kamati
hiyo  ya maliasili ya kijiji .

Kijiji cha  Limamu  na kilangalanga  kupitia mikutano yao ya hadhara
kwa wananchi wamepitisha mpango wa jamii wa usimamizi wa misitu katika
vijiji vyao ambapo  serikali  kupitia mpango huo  unawawezesha
wajumbe wa kamati  kuwapatia mafunzo  ili waweze kuusimamia vyema
mpango  huo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2