Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jamii mkoani Njombe na kwingineko hapa nchini imetakiwa kuwa na moyo wa huruma kwa kuwasaidia watu wasio jiweza ili kuhakikisha nao wanafuaraha kutokana na ukaribu unaojengwa katika jamii.
Wito umetolewa na Inspector Joel Mwakanyasa kutoka jeshi la zima moto mkoani Njombe walipotembelea kituo cha watoto yatima cha Tumaini Ilunda ili kujumuika nao katika kuunza vyema mwaka 2021 huku akitoa wito kwa taasisi nyingine za kiserikali na binafsi kuona namna ya kugusa makundi mbalimbali ndani ya jamii ambayo yanahitaji msaada.
“ tumepanga malengo yetu kila mwaka kwa ajili ya kuwafariji watu wenye makundi maalum,tunaziasa taasisi zingine za kiserikali kwasababu hii ni njia ya kutoa huduma kwenye jamii yetu”alisema Joel Mwakanyasa
Sister Magret Moyo ni mlezi wa kituo hiki ambaye anakiri ujio wa wahisani katika kituo hicho umekuwa msaada mkubwa na unatia faraja hasa kwa watoto yatima waishio katika kituo hicho ambao wengine wamepoteza wazazi na wengine kuokotwa baada ya kutelekezwa na wazazi wao huku akiitaka jamii kuacha tabia ya kutelekeza watoto.
“Kwanza tunashukuru kwa msaada ambao tumeupata na tunatoa wito kwa jamii waendelee kuwatunza watoto vizuri badala ya kuwatupa na kuwaweka kwenye mazingira hatarishi hasa vijana kwasababu wasichana wengi wanapokuwa kwenye mazingira magumu basi wanachukua uamuzi wa kuwatelekeza watoto”alisema Sister Magret Moyo
Jeshi la zimamoto mkoani Njombe limekuwa na utaratibu wa kutembelea watu wanaohitaji msaada maalumu ili kuendelea kutoa huduma kwa jamii ambapo zaidi ya mahitaji kama mafuta ya kupikia,juice,unga,mchele vyenye thamani ya zaidi ya laki mbili vimekabidhiwa kwa kituo hicho.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment