Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeisitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Televisheni ya Wasafi TV kwa muda wa miezi 6 kuanzia Januari 6 mwaka huu hadi Juni 2021 kwa makosa ya kukiuka taratibu za utangazaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Johannes Kalungula, amesema maamuzi hayo yanakuja kufuatia kipindi cha "Tumewasha Concert," Wasafi Tv cha Januari Mosi, 2021 majira ya saa mbili hadi saa tano usiku iliyorusha maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva Gift Stanford Mwakyusa maarufu kama Giggy Money akicheza katika jukwaa kwa mitindo iliyokuwa ikionesha utupu wa mwili wake kinyume na kanuni namba 11 (1) (b) (c) na (d) za kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta (Maudhui ya utangazaji wa Redio na Televisheni,) ya mwaka 2018 inayomtaka mtoa huduma wa maudhui kuhakikisha kuwa hatangazi maudhui yasiyozingatia utu na maadili ya Jamii.
Aidha Wasafi TV wametakiwa kutumia siku ya leo iliyobaki kuahirisha matangazo yote na kutumia muda wote uliobaki siku ya leo kuomba radhi kwa Umma wa watanzania wake kufuatia ukiukaji wa kanuni za utangazaji kupitia kipindi cha "Tumewasha Live Concert." Na wakikaidi au kukataa hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa dhidi ya Wasafi TV.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment