MAALIM SEIF ASEMA MARIDHIANO YA ZANZIBAR NI MTOTO ANAEHITAJI MALEZI BORA ZAIDI ILI AENDELEE KUWEPO. | Tarimo Blog

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad ameyasema hayo katika Mkutano wa ZANZIBAR PEACE CONFERENCE ambao umeandaliwa na taasisi ya FRIENDS OF ZANZIBAR wakishirikiana na Ofisi ya Mufti Zanzibar leo tarehe 16/01/2021.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort iliyopo Mazizini Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, umewakutanisha Wawakilishi wa kibalozi na taasisi nyengine mbalimbali ambao ni wajumbe wa taasisi ya Friend of Zanzibar.

Wawakilishi hao wametoa salamu zao sambamba na kusema kwamba wao wapo pamoja na Taifa la Zanzibar na wanawapongeza sana Viongozi kwa kushirikiana na kuleta amani katika Nchi hii.

Pamoja na hayo wageni hao wamesema hata wao wanaamini kwamba ushirikiano uliopo Zanzibar kwa sasa ni ujumbe mzuri kwa Mataifa mengine mengi ya bara la Africa.

Nae Maalim Seif katika kutoa salamu zake kwa Wajumbe hao alisema;
 "Katika Nchi mbalimbali migogoro huwa haiachi kutokea, lakini inapotokea kuna njia mbili hutumika, ya kwanza nikupigana hadi kuumizana ndio mwisho viongozi hukaa kwenye meza kutafuta suluhu, na nyengine ni kuepuka kugombana na mukakaa kwenye meza kuyatatua, na sisi Zanzibar tuliamua kukaa kwenye meza moja kuyajadili bila ya kuumizana na ndio njia nzuri zaid".

Maalim alitoa nasaha zake kwa Mgeni rasmi wa Mutano huo Rais Mwinyi kwa kumwambia;
"Mh. Rais maridhiano nikama mtoto ambae ni mwema, hivyo tunahitaji kumlea vyema ili vizazi vyetu vije kuirithi amani hii sambamba na kuiacha Zanzibar kuwa ni Nchi ya amani na iliyo salama".

Mwisho Maalim Seif  aliwashukuru sana taasisi ya Friend wa Zanzibar kwakusema;

 "Anaekufaa kwa dhiki ndio rafiki, na taasisi hii iliyokusanya wajumbe wa Mataifa mbalimbali nawashukuru sana kuwa pamoja nasi na kuendelea kuwa marafiki zetu hata wakati wa matatizo".







Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2