Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla ameelezea kuridhika kwake na matayarisho mazuri yanayoendelea kufanywa ya Tamasha la 7 la Biashara Zanzibar yakiwa ndani ya shamra shamra za Maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi Matukufu ta Zanzibar kutimia Miaka 57.
Hemed Suleiman alisema hayo alipofanya ziara fupi kukagua matayarisho ya mwisho ya Tamasha hilo akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar hapo Uwanja wa Maisara Suleiman ambapo uzinduzi wake utafanywa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Alisema inapendeza kuona Tamasha la Mwaka huu limedhaminiwa kwa gharama za Wadau wenyewe wa Maonyesho hayo kutoka Taasisi Binafsi pamoja na zile za Umma zinazohusinana na masuala ya Elimu na Biashara bila ya kuwemo nguvu za Serikali.
Alieleza kwamba Taasisi za Umma na hata zile Binafsi zinalazimika kubadilika katika matumizi ya fedha ili ziendane na mfumo halisi utakaozingatia utoaji wa huduma kwa Wananchi walio wengi.
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kwa kushirikisha Wadau moja kwa moja jambo lililosaidia kunusuru fedha nyingi kwenye maandalizi hayo.
Akijiridhisha na matayarisho hayo Hemed aliwataka Watendaji wa Taasisi za Umma zenye Vitengo vyao kwenye Tamasha hilo kuhakikisha kwamba wanawasaidia Zaidi Wananchi katika kuwapatia Elimu kuhusiana na huduma wanazotoa kwenye Taasisi zao.
Alisema zipo changamoto na malamiko mengi yanayolalamikiwa na Wananchi ambao wakati mwengine husumbuka kupata muwafaka wa malalamiko yao ambayo kwa kutumia Tamasha hilo baadhi yao yanaweza kupata msukumo wa ufumbuzi.
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Nd. Juma Hassan Reli Tamasha hilo linalofanyika kila Mwaka ndani ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar hutoa fursa ya kuuza na kununua likilenga kujikita Zaidi katika Uchumi endelevu.
Nd. Juma alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba jumla ya Washiriki Mia 340 wamejitokeza kushiriki Tamasha hilo wengi wa kutoka Taasisi Binafsi pamoja na zile za Umma.
Alifahamisha kwamba Washiriki wengi wa Tamasha hilo ambao ni Wafanyabiashara wa bidhaa tofauti wamepunguza malalamiko yao kama inavyotokea katika Matamasha yaliyopita kutokana na mpangilio bora wa mabanda ya Mwaka huu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment