MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MAGUFULI NA RAIS MWINYI CHATO. | Tarimo Blog

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi, katika Ikulu ndogo ya Chato Mkoa wa Geita.

Maalim Seif amefika mapema leo asubuhi tarehehe 14/01/2021, katika uwanja wa ndege wa Mwanza  na kupokelewa na Viongozi waandamizi wa Kiserikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza Mh. Sevelin Lalika.

Maalim Seif alipata fursa ya kutembelea ujenzi wa Daraja la Magufuli lililopo Kigongo feri Mpakani mwa Misungwi na Sengerema.

Mradi wa daraja hilo ukikamilika utaleta mafanikio makubwa ya kuunganisha baadhi mikoa ya Tanzania pamoja na kuunganisha Tanzania na Nchi jirani kama Burudi,Rwanda na Congo.

Baada ya Ziara hio Maalim Seif alifika Chato kwenda kukutana na Marais hao ambao walijadili mambo mengi na baadae kuzungumza na umma wa Watazaznia na Dunia kwa Ujumla kupitia waandishi wa habari.

Katika mkutano na waandishi wa habari Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar alisema;

”Tumebadilishana mawazo juu ya mustakbali wetu wa Zanzibar na namna bora zaidi ambavyo tunaweza kuwatumikia Watanzania”.

Katika kusisitiza hilo Makamu wa kwanza amesisitiza yakwamba;

"Kwanamna tulivyo zungumza na kukubaliana inaonesha wazi Rais Magufuli anania njema ya kutuunga mkono na kuyaboresha maisha ya Wazanzibar wa kisiwa cha Pemba na Unguja".








 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2