MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA MKUU WA JKT CHARLES MBUGE KATIKA SKIMU YA UMWAGILIAJI YA KIKOSI CHA CHITA JKT 837 | Tarimo Blog


 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akifurahia jambo na Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa wanaojenga miundombinu ya Skimu ya umwagiliaji ya Kikosi cha Chita JKT 837 uliopo Ifakara Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akiangalia jinsi maji yanavyopita katika moja ya banio ambalo litatumika kugawa Maji kwenda katika mashamba ya mpunga katika mradi wa umwagilkiaji unaojengwa na kikosi cha 837 Chita JKT Ifakara,Mkoani Morogoro.


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja General Charles Mbuge akitembelea moja ya ghala embalo litatumika kuhifadhia mpunga utakaovunwa katika mashamba hayo ya kimkakati wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya mradi huo uliopo Ifakara Mkoani Morogoro.
:Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge  akiangalia moja ya mfereji wa kupeleka maji  unaojengwa katika skimu ya umwagiliaji ya Chita JKT kikosi 837 Chita JKT, unaopita chini ya reli unaopeleka maji katika  mashamba ya mpunga  wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya mradi huo   Ifakara Mkoani Morogoro.Ujenzi wa miundombinu ya skimu hiyo umefikia asilimia 45 na unategemea kukamilika mwezi Mei 2021.
Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Meja General Charles Mbuge akiangalia sehemu ya ekari 2500 zilizopandwa mpunga na kikosi cha 837 Chita JKT  wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya mradi huo uliopo Ifakara mkoani Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge  akiangalia moja ya mfereji wa kupeleka maji  unaojengwa katika skimu ya umwagiliaji ya Chita JKT kikosi 837 Chita JKT, unaopita chini ya reli unaopeleka maji katika  mashamba ya mpunga  wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya mradi huo   Ifakara Mkoani Morogoro.Ujenzi wa miundombinu ya skimu hiyo umefikia asilimia 45 na unategemea kukamilika mwezi Mei 2021.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2