TAASISI ya uhasibu Nchini (TIA,)kwa kushirikiana na kampuni ya Golden Nation wametoa mafunzo maalumu kupitia jukwaa la ''Mind set event'' kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini yakilenga kuwajengea uwezo kufanya maamuzi na fikra zaidi katika kujiandaa na safari pindi wamalizapo masomo yao na kurejea katika jamii.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya Golden Nation Lameck John amesema kuwa, lazima vijana wafikiri zaidi ni nini watafanya kwa jamii yao kwa baadaye na kuwataka vijana hao kuwa na malengo na kuzitumia fursa zaidi na sio kufikiri katika kuajiriwa pekee.
''Kwa hatua tuliyofikia hapa lazima tuoneshe ukomavu wa fikra kwa kuchakata maarifa tuliyopewa darasani kwa kuyahusianisha na fursa zilizopo katika jamii, na hiyo ni kwa kushirikiana na walimu pamoja na sisi vijana kwa kuhakikisha kuwa tunashikana mikono na kila mmoja wetu anatimiza ndoto zake.'' Amesema.
Aidha amewashauri wanavyuo hao kutumia fursa zitokanazo na mitandao ya kijamii kutimiza malengo yao na hiyo ni pamoja na kusoma pamoja na kutangaza masuala yenye tija kwao na jamii kwa ujumla.
Vilevile ameeleza kuwa, ushirikiano ya wahitimu una nguvu katika kuhakikisha maendeleo na mafanikio yanafikiwa kwa kila mmoja bila kutegemea ajira za moja kwa moja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jeannelle Corporate Solution Jeremia Kahurananga amewashauri wanavyuo hao kuweka mbele na kuendelea kupata elimu ya utambuzi ili waweze kufanya mambo makubwa zaidi wanayowaza kuyafanya.
''Elimu haina mwisho, na kwa hatua hii mliyofikia ni vyema mkawa mnahudhuria warsha za aina hii ambazo kwa kiasi kikubwa zinawaandaa na namna ya kukabiriana na changamoto za ajira.....ukipata somo katika warsha hizi unaweza kujiandaa vizuri kifikra kwa kutotegemea ajira za moja kwa moja bali kujiajiri wewe mwenyewe,'' Amesema.
Kahurananga amekishukuru Chuo cha TIA kwa kuendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo kwa wanafunzi wao na kusema kuwa hafla hiyo iliyoandaliwa na Chuo hicho kwa kushirikiana na Golden Nation itumike kama chachu kwao na vyuo vingine kwa kuwafanya vijana kufikiri zaidi ni nini watafanya kwa manufaa yao jamii na vijana katika jamii.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment