MBUNGE ZEDI AFUNGUKA KAMATI YA LAAC KUANZA MAFUNZO YA WIKI MOJA | Tarimo Blog

Charles James, Michuzi TV

Kamati ya LAAC imeteuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, na leo hii wajumbe wa kamati hiyo wameanza kupewa mafunzo ya wiki moja ya kuwajengea uwezo ili waweze kusimamia matumizi ya rasilimali za umma zinazopelekwa kwenye Halmashauri zetu zote 185 Tanzania.

Akizungumza jijini Dodoma Makamu Mwenyekiti wa LAAC ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukene, Selemani Zedi amesema watayatumia mafunzo hayo kikamilifu katika kuwatumikia watanzania

" Kwa mujibu wa majukumu yetu kikanuni, tutahakikisha rasilimali za umma zinazopelekwa halmashauri zinatumika kama zilivyokusudiwa, na matumizi yote yanafanyika kwa mujibu wa sheria ya fedha ya Serikali za Mitaa.

Kama ambavyo tuliapa kuilinda Katiba yetu na kuwaahidi wananchi wetu kuwatumikia kwa nguvu zetu ndivyo tutakavyozilinda rasilimali zetu kwa wivu mkubwa," Amesema Mbunge Zedi.


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2