NA YEREMIAS NGERANGERA..NAMTUMBO.
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Juma Pandu amewataka watumishi wa serikali katika halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao na kuongeza ushirikiano katika kazi.
Pandu aliyasema hayo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo akiwa na wakuu wa idara na vitengo kueleza changamoto alizozibaini katika ziara yake ya kukagua miradi katika Halmashauri hiyo na kuwataka watumishi kuwajibika katika nafasi zao na kuongeza ushirikiano ili kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayoikabili jamii .
Aidha bwana Pandu aliwaambia wakuu wa idara na vitengo anapenda kuona ushirikiano kutoka kwa wakuu wa idara na vitengo pamoja na waheshimiwa madiwani kwa kufanya hivyo wataweza kutatua changamoto zilizopo katika jamii kwa pamoja.
Alitaja changamoto ya uhaba wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya ,watumishi wachache wa idara ya afya na kumwagiza mkuu wa idara ya afya kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati na huduma zitolewa nzuri kwa wagonjwa alisema bwana Pandu.
Changamoto ya ujenzi wa maboma kwa nguvu za wananchi wenyewe kama madarasa,vyoo,zahanati, bwana pandu alimtaka mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wataalamu wanafika katika maeneo yanakojengwa maboma hayo ili majengo yanayojengwa yawe na ubora wa kiwango cha serikali.
Diwani wa kata ya Limamu bwana Isdori Nyati katika kikao hicho alidai ucheleweshaji wa utoaji wa fedha kwa wajumbe kutoka vijijini unachukua muda mrefu na kutaka swala hilo liwekewe utaratibu ili kupunguza kero kwa wananchi wanaofuata huduma za kuchukua fedha.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Evance Nachimbinya pamoja na kuwashukuru wajumbe wa kikao hicho alisema wamepokea maagizo hayo na kwenda kuyafanyia kazi lakini utaratibu wa utoaji wa fedha za serikali utazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na sio vinginevyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment