Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoani Pwani ,Michael Mwakamo, amewaasa wadau na jamii kujenga tabia ya kuendelea na utamaduni wa kutembelea vituo vinavyolea watoto wenye mazingira hatarishi na kuvisaidia.
Ameeleza ,vituo hivyo vimejitolea na si kama vyote vinajiweza kila kitu na kama ni kwa kila kitu lakini inastahili jamii ikajitoa na kushirikiana kusaidiana kwani watoto hao wanahitaji mahitaji muhimu kama walivyo wengine.
Mwakamo ametoa rai hiyo kwenye chakula cha pamoja na kituo cha Masjud Nour cha Mlandizi, kilichoandaliwa na ofisi yake akishirikiana na wadau mbalimbali, ambapo watu kadhaa walihudhulia hafla hiyo ikiwa ni kuukaribisha mwaka mpya.
"Hawa ni vijana wetu wanaolelewa katika kituo hiki na vingine vilivyopo jimboni kwetu, nao walikuwa na wazazi kama sisi lakini kwa mapenzi ya mungu sasa hawana hivyo kulelewa na vituo hivi, hivyo niwaombe tuvitembelea na kuvisaidia," alisema Mwakamo.
Aidha alisema kwamba akiwa Mtendaji Kata maeneo mbalimbali alikuwa anaagizwa na viongozi waliokuwa juu yake, lakini sasa amekuwa Mbunge hivyo anatambua fika changamoto zilizopo na kwamba anawaomba wakazi wa ndani na nje ya Jimbo kuvitembelea na kuvisaidia.
Awali kiongozi wa kituo hicho ,Seif Wenge alieleza changamoto ya kukosekana kwa uzio, hali inayochangia watu kukatisha wakati wowote.
"Kituo chetu kilianzia Kilngalanga, baadae jirani na soko la Mlandizi kabla ya kujenga majengo haya mnayoyaona haya ni mafanikio lakini bado tuna changamoto tunaomba wadu wake kuvisaidia," taarifa ya Wenge ilielezea taarifa hiyo.
Alisema kwamba katika sekta ya elimu kituo kimetoa wanafunzi wawili ambapo wamefaulu na kutakiwa kuanza elimu ya sekondari kuanzia mwaka wa 2021, ambapo wanahitaji vifaa mbalimbali vinavyohitajika katika masomo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment