RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE WA BARAZA LA TAIFA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA CHINA WANG YI IKULU NDOGO YA CHATO MKOANI GEITA | Tarimo Blog

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi kabla ya kuanza mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji Saini wa mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Masanja Kungu Kadogosa  na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC kupitia Mtendaji Mkuu wa CCECC Zhang Junle  katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi wakati akizungumza mara baada ya utiaji saini wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi wakati wakielekea kupata chakula cha mchana katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akiongoza mazungumzo kwa upande wa Tanzania pamoja na Ujumbe wa Kutoka China uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi katika Ikulu ndogo ya Chato.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mara baada ya kuzungumza na wageni mbalimbali katika hafla fupi ya utiaji saini wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wadogo wadogo wamachinga na kuwapa zawadi Waandishi wa Habari waliokuwepo katika ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo kuhusu zawadi ya Kinyago cha mti wa Mpingo kwa Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ili akiwasilishe kwa Rais wa China Xi Jinping mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake hapa nchini.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2