TANESCO YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAMILIKI WA VIWANDA NA MASHINE ZA KUSAGA MKOANI RUKWA | Tarimo Blog


NA Neema Mbuja, Rukwa

Shirika la umeme Tanzania TANESCO kupitia Idara ya masoko imeendelea na kampeni ya kutoa Elimu kwa wamiliki wa viwanda,machimbo ya madini, na mashine za kusaga kwa mkoa wa Rukwa ili kuwapatia Elimu juu ya matumizi Bora ya umeme sanjari na kukagua miundo mbinu ya umeme pamoja na mota zinazotumiwa kwenye kuendesha mashine viwandani

Miongoni mwa Elimu wanayopatiwa Ni pamoja na namna ya kutumia vifaa ambavyo vinatumia umeme kidogo, umuhimu wa kukagua mota zao Mara kwa Mara kwa ajili ya kuleta ufanisi na Usalama wa miundo mbinu ya TANESCO kwenye maeneo yao

Akizungumza na wamiliki wa viwanda kwenye Wilaya za Sumbawanga mjini na Laela , mhandisi kutoka  kutoka idara ya utafiti Baraka Kanyika  amesema kuwa kwa Sasa baadhi ya  viwanda vinatambua umuhimu wa kufunga power factor ingawa baadhi bado hawajatambua

Kuhusu wamiliki wa mashine  za kusaga Kijiji Cha muze Wilaya ya Laela mkoa wa Rukwa mhandisi Kanyika ameshauri kuendelea kuwapatia Elimu ya umuhimu wa kukagua mota zinazoendesha mashine zao Mara kwa Mara ili kuziongezea ufanisi wa utendaji kàzi na kulinda miundo mbinu ya shirika.









<
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2