TCRA yawanoa Polisi mkoani Pwani kuhusu Makosa ya Kimtandao | Tarimo Blog


*Jeshi la Polisi Pwani laahidi ushirikiano katika kukabiliana na uhalifu wa kimtandao .

Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv Pwani
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limesema kuwa litaendelea na kwenda na mbinu mbalimbali katika kukabiliana na Makosa ya Kimtandao (Cyber Crime).

Akizungumza katika mafunzo kwa askari wa Makosa ya Kimtandao  iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki, kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Mnadhimu wa Polisi ACP Gregory Mushi amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani wahalifu wanambinu nyingi hivyo kukutana na TCRA kunajenga uimara katika kukabiliana na wahalilifu hao.

ACP Mushi amesema kuwa Askari wakipata mafunzo watajua namna ya kuhudumia wanannchi wanaokuwa wamepata  changamoto katika mawasiliano kwa kufanyiwa utapeli.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani tutaendelea kushirikiana  na TCRA katika utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kukabiliana na wahalifu wa Makosa ya Kimtandao na kuwafikisha katika vyombo vya sheria"amesema Mushi.

Nae Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi  Lawi Odiero amesema kuwa utoaji elimu ni endelevu kwani kadri ya Teknolojia inavyobadilika ndivyo wahalifu wanabuni mbinu zingine.

Amesema kuwa TCRA imejipanga katika kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali katika kwenda sambamba na ukuaji wa Teknolojia ya Mawasiliano.

Mhandisi Odiero amesema wananchi wanatakiwa wanapofika Polisi wanapata huduma kwa mujibu wa sheria.

Kwa Upande wa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Joshua Mwangasa amesema kuwa kutokana na elimu Makosa yanapungua kwani kwa miaka miwili imefikia wahalifu 3000.
Amesema hakuna mtu atakayeachwa kutokana na Makosa ya Kimtandao hata kwa watoa huduma.

Amesema kuwa Askari kwa mafunzo waliyoyapata watatoa huduma bora kwa wananchi wanapofika katika Makosa ya kimtandao.

Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Gregory Mushi akizungumza na Askari wakati akifungua semina ya mafunzo kwa Askari hao ya kufanya tathimini na ufatiliaji wa Makosa ya Mtandao iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero  akizungumza kuhusiana  mafunzo Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani namna ya kukabiliana na Makosa ya kimtandao kwa watumiaji kufanya uhalifu.
Mhandisi wa Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Christopher John akitoa mada katika mafunzo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.
Mwanasheria Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Vaolet Eseko akitoa mada za kisheria kuhusiana na Makosa ya kimtandao kwa Askari wa Jeshi Polisi mkoani Pwani.

 

Baadhi ya Polisi wakiwa katika mafunzo ya kufanya tathimini na  ufatiliaji  ya Makosa ya Kimtandao .


 

 Picha ya Pamoja ya Mgeni Rasmi,Wafanyakazi wa TCRA na Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2