KAIMU Msajili wa Bodi ya Maziwa Ndugu, Noely Byamungu ametoa rai kwa wawekezaji nchini kuwekeza kwenye ufugaji wa Ngo'mbe bora Maziwa ili kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini.
Hayo amesema jana (6.1.2021) wakati alipomtembelea mwekezaji wa shamba la Ng'ombe wa Maziwa la Shafa lililopo jijini Iringa.
Ndugu Byamungu amesema kuna fursa kubwa katika ufugaji wa ngo'mbe wa maziwa na hivyo wawekezaji hawana budi kuwekeza kwenye ufugaji wa ng'ombe bora wa kisasa wanaozalisha maziwa mengi.
Ndugu Byamungu alisema hadi sasa uzalishaji wa maziwa nchini umefika lita bilioni 3.0 tu kutokana na ufugaji wa ng'ombe wa asili.
Kati ya lita hizo, lita bilioni 2.1zinatokana .net ngo'mbe wa asili na lita bilioni 0.9 za maziwa zinatokana na ngo'mbe wa kisasa.
Natoa wito kwa wadau wa sekta ya maziwa kuwekeza kwenye ufugaji wa Ng'ombe wa kisasa ili kuongeza uzalishaji" Alisema Byamungu
Sambamba na hilo Byamungu alimpongeza mwekezaji huyo kwa jitihada kubwa alizofanya za kuinua Tasnia ya Maziwa nchini kupitia ufugaji wa ng'ombe bora wa kisasa wa maziwa.
Nae Mwekezaji wa Shamba la Shafa Ndugu, Mohammed Al -Alhazi ameishukuru Bodi ya Maziwa kwa kutembelea shamba lake na kwamba huu utakuwa mwanzo mzuri wa Bodi kujenga mahusiano mazuri na wadau.
" Sisi kama wawekezaji tunashukuru sana bodi ya maziwa kwa ushirikiano huu mnaoendelea kutupatia" Alisema
Amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni usalama wa mifugo kwani wananchi hupita kwenye eneo la Shamba hali inayoweza kusababisha magonjwa ya mlipuko na hivyo kuhatarisha afya ya mifugo.
Aidha , Mwekezaji huyo amesema lengo la shamba ni kuwa na Shamba bora la ngo'mbe wa maziwa Afrika Mashariki kwa kuongeza idadi ya ng'ombe wa maziwa kutoka 400 waliopo hivi sasa hadi 1000 ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Shamba la Shafa lilianzishwa mwaka 2019 likiwa na takribani ya ngo'mbe wa maziwa 120 tu.
Hadi sasa shamba hilo lenye ekari 2500 lina ndama 142 na ng'ombe wa maziwa wapatao 400 wanaotoa wastani wa Lita 27 za maziwa kwa ng'ombe na hivyo kufanya jumla ya Lita 7500 za maziwa kukamuliwa kwa siku.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Ndugu, Noely Byamungu ( kulia) akiwa kwenye kikao na mwekezaji wa Shamba la Ng'ombe wa Maziwa la Shafa Ndugu, Mohammed Al-Alhazi (kushoto) na timu ya wataalamu wa Bodi ya Maziwa (hawapo pichani) tarehe (6.1.2021) kwa lengo la kuangalia uzalishaji wa maziwa unaofanywa na Mwekezaji huyo mkoani Iringa.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Ndugu, Noely Byamungu ( wa kwanza kushoto) akipata maelezo ya utunzaji wa ng'ombe kutoka kwa Ndugu, Mohammed Al- Alhazi ( katikati) wakati alipotembelea shamba hilo lenye ng'ombe takribani 400 wanaozalisha maziwa Lita 7500 kwa siku. Wa kwanza kulia ni Afisa Usindikaji Bodi ya Maziwa, Bi. Fathiya Rashid.
Baadhi ya Ng'ombe wakiwa katika maeneo yanapofugwa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment